FAHAMU KUHUSU ULINZI WA RAIS WA MAREKANI

0:00

MAKALA

Unaweza kujiuliza Taifa kubwa ambalo limewahi kuwashuhudia maraisi wake wanne wakiuwawa mbele ya macho yao, licha ya ulinzi mkali litakuwa ‘serious’ kiasi gani katika kuepukana na aibu hiyo.

Ukijiuliza hilo utafahamu kuwa suala la kumlinda rais wa Marekani si la kupuuza.

Leo nakulete siri kuhusu walinzi wa Rais wa Marekani wafahamikao kama ‘Secret Services’ yaani Huduma za Siri, au unaweza kuwaita Usalama wa Taifa kama ilivyozoeleka kwa watu wengi.

Kama unavyofahamu kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu walinzi wa maraisi hasa kuhusu uwezo wao na njia wanazotumia kumlinda raisi.

Lakini leo nikujulishe njia mbali mbali wanazotumia walinzi hawa wa Rais wa Marekani

1. Maktaba ya Wino.

Inawezekana unahisi umejificha sana lakini ni ukwel usiopingika kuwa ‘Secret Services’ wanaweza kukupata popote ulipo endapo utajaribu kujifanya una akili sana kwa kutotumia simu, computer au kifaa chochote cha ki-electeonic kutuma vitisho juu ya Rais na ukaamua kutumia barua iliyoandikwa kwa mkono.

Hapo utakuwa umejidanganya, Idara ya Ulinzi wa Rais wa Marekani imekuwa na Maktaba ya wino iliyotengenezwa na kampuni zote duniani ambazo hupeleka ‘samples’ za kila aina ya wino na kueleza kuwa ‘sample hiyo itapelekwa nchi fulani.

Hivyo wino katika ‘pen’ zote duniani sample yake ipo katika maktaba ya ‘Secret Services’, na endapo barua yoyote ya vitisho itafika mezani kwa Rais, basi moja kwa moja basi wataalam huchunguza na kujua wino huo upo nchi gani na hivyo watakupata kirahisi.

Lakini hata ukitumia wino wa nchi nyengine ukiwa katika nchi yako, kitengo hiki kina wataalamu waliobobea katika kuchambua miandiko ya binadamu, lakini hata kama kuna ujumbe wa hatari uliofichwa chini ya barua yenye upendo kwa Rais, wataalam hawa wanaweza kutambua ujumbe huo na mara moja kukufatilia na hivyo watakupata tu.

2. Kitengo cha Mtandaoni.

Kiukweli Dunia sasa hivi imekuwa na wanajeshi wengi sana, watu mahiri wengi na wahamasishaji wengi lakini wote wapo nyuma ya vitufe vya simu zao na ‘computer’ zao.

Watu hawa wamekuwa wakitukana na kuwatisha watu wengine huku wakihamasisha mambo mbali mbali kwa kutumia vifaa vyao kama simu na computer.

Hivyo kwa mtu ambae anafahamika dunia nzima, na ambae maamuzi yake yanawaathiri hata binadamu wasio katika nchi yake kama Rais wa Marekani, lazima atapokea vitisho na jumbe mbali mbali za kumdhuru au kuonesha jinsi gani kuna shambulio la kumdhuru linataka kutokea dhidi yake.

See also  Neymar suspects latest injury nothing more serious than cramp

Kwa kutambua hilo, ‘Secret Services’ wana kitengo maalum kwa ajili ya kufatilia kila jumbe za mtandaoni ambazo zinaonyesha kuna shambulio fulani dhidi ya Rais.

Lakini pia si kila jumbe huchunguzwa kwani Maofisa wa kitengo hiki wana uwezo wa kujua kama ujumbe ‘fulani’ ni ‘serious’ ama sio ‘serious’.

Lakini endapo mtu yoyote ata-post chochote ambacho Maofisa hawa wataona ni hatarishi kwa usalama wa Rais basi mara moja kila taarifa kuhusu mtu huyu zitachunguzwa, watahojiwa watu wake wa karibu, majirani, wafanyakazi wenziwe, hata walimu waliomfundisha na baada ya hapo hatua zitakazofuata zitaangaliwa kama mtu huyo aonywe, achukuliwe kwa mahojiano zaidi au ahukumiwe kwa kosa hilo.

3. Chakula Cha Rais.

Inawezekana ushawahi kuona Marais mbali mbali wa Marekani wakijiachia na misosi katika migahawa mbali mbali wanapokuwepo katika matembezi.

Lakini nikueleze ukweli kuwa matokeo yale yanakuwa kwa ajili ya picha tu, kwa sababu Rais haruhusiwi kula chochote wakati kinatayarishwa maafisa hawa hawakuona kwa macho yao.

Hivyo kabla ya Rais wa Marekani hajaenda katika mgahawa wowote, Maafisa hawa hufika na wapishi maalum na kuandaa chakula hicho, hivyo Rais huonekana kama amenunua chakula hicho hapo hapo mgahawani lakini ukweli ni kwamba sio isipokuwa chakula hicho kimeandaliwa hapo na Maafisa Usalama.

Lakini si Mgahawani tu hata chakula ambacho Rais wa Marekani atakula anakuwepo ‘White House’ au ndani ya ndege yake ‘Airforce One’, kinaandaliwa na wapishi wa kijeshi ambao pia watakuwa katika uangalizi mkali wa ‘Secret Services’ na hata baada ya chakula kuiva hupimwa kuhakikisha hakuna sumu inayoweza kumdhuru Rais.

4. Uwezo wa Kuona Silaha iliyofichwa.

Moja katika zoezi gumu walilonalo maofisa wa ‘Secret Services’ ni kumlinda Rais awapo katika maeneo ya watu wengi kwani lolote laweza kutokea kutoka kwa maadui waliojichanganya katika umati wa watu wema waliokuja kumlaki Rais.

Hivyo katika kutambua hilo, Maofisa wa ‘Secret Services’ huwa makini sana kuwatazama watu na kuweka umakini mkubwa kwa yeyote anaeonekana kutia shaka kwa mienendo yake.

Maafisa hawa huweza kumjua mtu alieficha silaha kwa kutazama jinsi anavyotembea, alivyoweka mikono na wale waliovaa nguo pana kupitiliza, kwani wana uwezo mkubwa wa kuficha silaha ndani ya nguo hizo.

Mara ngingi Maafisa hawa huvaa miwani, lakini ukweli ni kwamba miwani hiyo yenye rangi nyeusi hawaivai kuwafanya wapendeze au kuwafanya waonekane wanatisha.

La hasha! Mara nyingi wamekuwa wakivaa miwani hiyo meusi ili kuzuia miale ya jua inayoweza kuwafanya wasione vizuri hatari yoyote inayotaka kujitokeza.

See also  𝗞uhusu Usajili wa JEAN 𝗕𝗔𝗟𝗘𝗞𝗘 Yanga na Uchambuzi wa Nafasi Yake Kama Mshambuliaji

Lakini kubwa zaidi ni kufanya macho yao yasionekane yanaangalia upande gani, hivyo wakati adui akidhani afisa huyu anatazama upande mwengine kumbe vile macho ya Afisa huyu yapo kwake na kabla hajafanya shambulio anakuwa tayari keshadhibitiwa.

5. ‘CAT’ Agency.

Ninaposema ‘Cat Agency’ simaanishi mnyama yule paka (nyau), bali namaanisha ‘Counter Assault Team’. Hiki ni kikosi ndani ya ‘Secret Services’ ambacho mara nyingi Maafisa hawa huvalia nguo kama ‘Combat’ (Magwanda ya Kijeshi) na Maafisa hawa hupitia mafunzo maalum ndani ya miezi kadhaa na baada ya kufaulu ndipo huweza kuingia kwenye ‘team’ hii ambayo huwepo popote atakapokuwepo Rais wa Marekani.

Afisa yeyote aliepo katika ‘CAT Agency’ lazima awe na uwezo mkubwa wa kupambana kwa kutumia silaha za aina mbali mbali na ndio maana muda mwingi wanakuwa wamebeba silaha na silaha hizi ni moja kati ya silaha zenye nguvu sana.

Ikae akilini mwako kuwa ujuzi wa kupambana na silaha pekee hauwatoshi maafisa hawa, hivyo wanatakiwa kuwa na uwezo wa kupambana bila hata ya silaha.

Nimekueleza tu sifa zao, bado sijakuambia kazi zao wawapo katika msafara wa Rais. Lakini kabla sijakueleza nikukumbushe tu kuwa wanaitwa ‘Counter Assault Team’, maana yake hawa kazi yao ni kulishuhulikia tatizo papo hapo.

Hivyo kuwapo na shambulio lolote Maafisa hawa kazi yao ni kuendelea kupambana na adui ili kuwapa nafasi maafisa waliomzunguka Rais wamkimbize Rais na kumuondoa eneo la tukio.

Hivyo Maafisa hawa huwa mstari wa mbele kabisa kuwalinda Maafisa wengine wanaomlinda Rais.

6. Advanced Secret Service Dean.

Wengi tumezoea kutumia neno ‘Advance’ kama malipo ya awali kabla ya kumaliziwa kwa malipo mengine, sasa tumia uwelewa huo katika eneo hili.

Advanced Secret Service Dean ni Maafisa Usalama wa Rais ambao hutangulia eneo lolote kabla ya Rais hajawasili na kazi yao ni kuhakikisha wanakagua kila kitu katika eneo hilo na maeneo mengine yanayozunguka eneo hilo ili kuhakikisha kila kitu ni salama eneo hilo.

Kwa mfano kama Rais anataka kwenda kwenye shule ya watoto, hivyo maafisa hawa hutangulia na kukagua kila kitu ikiwemo majengo ya karibu.

Na endapo kuna hospital karibu, basi Maafisa hawa hutaka kujua idadi ya wagonjwa waliokuja hivi karibuni na endapo kuna mgonjwa yeyote mwenye matatizo ya akili basi maafisa hawa pia watataka wafahamu.

Na endapo Raisi atafika katika Hotel fulani basi Maafisa hawa hufika kabla na kufatilia historia za wahudumu wa hotel hiyo, na kama kuna mhudumu ana historia ya uhalifu basi siku atakayofika Rais, mhudumu huyo hatatakiwa kuwepo.

See also  Portugal Coach praises squad's progress since Euro 2024 exit

Maofisa hao huchukuwa vyumba katika ‘floor’ nzima atakayokuwa Rais bila kusahau floor ya chini yake na ya juu yake, wakati mwengine huchukuwa hata ‘elevator’ au ‘lift’ kama wengi tulivyozoea kuita na lift hii hutumika kwa matumizi hayo ya kiusalama.

7. The 10 Minutes Medicine.

Hii kanuni ambayo kusudio lake ni kuhakikisha kwamba Rais anapata msaada wa kimatibabu ndani ya dakika 10 za kwanza baada ya shambulio au hata matatizo ya kawaida ya kiafya.

Hivyo Maafisa hawa kutoka katika Kitengo cha kumlinda Rais maarufu kama ‘Presidential Protective Division’ (PPD), licha ya kuwa na uwezo wa kutoa huduma ya kwanza Maafisa hawa wanatakiwa kuhakikisha kwamba begi za damu zenye kundi moja na damu ya Rais zinakuwa kwenye gari ambayo Rais anapanda muda wote yaani namaanisha ‘The Beast’ na hutumika endapo Rais atatakiwa kuongezewa damu kwa sababu yoyote ile.

Licha ya hilo, Maafisa hawa watatakiwa kujua katika eneo aliopo Rais ni hospital gani ilipo karibu kwa mwendo wa ‘Dakika 10’.

Lakini usidhani kuwa Hospital hiyo itaachwa hivi hivi, lakini kabla ya Rais kufika hapo, kuna Maafisa hupandikizwa kwa ajili ya kufatilia historia za ‘Ma-nurse’ na madaktari wote katika hospital hiyo na hasa wale watakaokuwa katika ‘Shift’ ambayo Rais atakuwa katika eneo hilo.

Na endapo kuna mmoja kati ya ‘Doctor’ au ‘Nurse’ au mfanyakazi yoyote wa hospital hiyo ana historia inayotia mashaka basi mfanyakazi huyo hatatakiwa kuwepo.

8. Huduma za Siri.

Kama kikosi hicho kinavyoitwa ‘Secret Services’ basi nikueleze tu kwamba kuna mambo mengine mengi sana yanabaki kuwa siri.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

UNDERSTANDING COURTSHIP
For all the single men and ladies: Having encountered and interacted...
Read more
10 THINGS YOU MUST NOT DO DURING...
LOVE ❤ 1. Looking at time when you are having...
Read more
UMUHIMU WA KUOA AU KUOLEWA NA MWENZA...
MAPENZI 1. MUNGU humpa maono ya kuingia kwenye ndoa na...
Read more
President Ruto's Cabinet Nominees Submitted to Parliament,...
President William Ruto has submitted a list of 11 Cabinet...
Read more
HESABU ZA AZAM FC ZIKO HIVI ZA...
MICHEZO Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo ameweka wazi...
Read more

Leave a Reply