MICHEZO
Rais wa FC Barcelona Joan Laporta amekiri kuwa klabu hiyo imekataa ofa ya Pauni milioni 200 (sawa na Sh bilioni 551) kwa ajili ya Lamine Yamal.
Taarifa hiyo imetolewa hivi karibuni, kupitia kwa wakala Jorge Mendes baada ya kutoa mapendekezo kuhusu mshambuliaji huyo wa Blaugrana.
FC Barcelona imekataa kabisa ofa kutoka klabu ya Ufaransa ya PSG kwa sababu wanafikiria mchezaji huyo atawafaa katika siku za usoni.
Hivi ndivyo jinsi Laporta alivyosema: “Tumepokea ofa kwa ajili ya baadhi ya wachezaji wetu, kama Lamine Yamal, kwa ada ya euro milioni 200, na alisema hapana. Kwa sababu tunamuamini kijana, kwa sababu ni nguzo ya timu hapo baadae.
“Kwa sababu tuna imani na kijana, ana kipaji, na bado tunamuhitaji,” alisema Laporta, ambaye alisema klabu hiyo inapitia kipindi kigumu kwa sasa.
Hali ya kifedha ya Barcelona sio nzuri sana, hivyo inashawishi kutaka kumuuza mchezaji huyo kwani kutasaidia kuipatia kipato cha fedha klabu hiyo kutoka kwa mhezaji wao mmoja na hiyo ni njia pekee ya kusaidia kuweka sawa matumizi ya fedha.