MICHEZO
Klabu za AC Milan na Juventus zinaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Fiorentina na Morocco, Sofyan Amrabat ambaye kwa sasa anaichezea Manchester United kwa mkopo.
Hadi sasa Man United haijaonyesha nia ya kutaka kumsainisha mkataba wa kudumu Amrabat aliyejiunga nao katika dirisha lililopita la majira ya baridi.
Amrabat alijiunga na Man United kwa mkopo uliokuwa na ada ya Euro 9 milioni na kuna kipengele cha kumnunua mazima kwa Euro 25 milioni.
Juventus ndio imeripotiwa kuwa ya kwanza kutaka kumsajili staa huyu lakini Milan nayo imeibuka katika siku za hivi karibuni, na ndio inaonekana kuwekeza nguvu kubwa zaidi.
Milan inataka kumsajili Amrabat kwa sababu inapitia changamoto eneo lao la kiungo hususani katika upande wa kuzuia.
Amrabat alitua Man United baada ya mashetani hao wekundu kushinda vita dhidi ya Barcelona.
Tangu atue Man Utd, kiungo huyu amecheza mechi 22 za michuano yote na Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.