MAKALA
Wanasayansi wanasema, hadi umri wa miaka 35, wanawake wengi hawana matatizo na uzazi, lakini baada ya umri huo uwezekano wa kupata mimba huanza kupungua kwa kasi.
Ni kweli kwamba wanawake wengi wenye umri wa zaidi ya miaka 35 hupata ugumu wa kushika mimba na wakati mwingine wako katika hatari zaidi ya matatizo yanayohusiana na ujauzito na uzazi kuliko wanawake wenye umri wa miaka 20 hadi 35.
Hata hivyo, kupungua kwa uwezo wa kupata mimba ni mchakato wa polepole sana, sio jambo la ghafla, na mchakato huo unatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine.
“Kuanzia umri wa miaka 35, ubora na wingi wa mayai hupungua kwa kasi,” anasema Lorraine Casavant, daktari wa uzazi na mtafiti katika Chuo cha Imperial London.
Lakini Profesa Anja Bisgaard Pinborg, mkuu wa idara ya uzazi katika kliniki ya Rigshospitalet huko Copenhagen, anasema, “wanawake wengi wana matatizo ya kupata mimba baada ya umri wa miaka 40, hata kama wanakoma hedhi wakiwa na umri wa wastani wa miaka 51.”
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.