WALIOFANYA SHAMBULIZI NCHINI URUSI WAKAMATWA WANNE

0:00

HABARI KUU

Serikali ya Urusi, imewafungulia mashtaka watu wanne wanaodaiwa kufanya shambulizi katika ukumbi wa Crocus City Hall jijini Moscow usiku wa kuamkia Machi 23, 2024 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 130 karibu na jiji la Moscow.

Watu hao wamefunguliwa mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny mjini Moscow ambapo huenda wakakabiliwa na hukumu ya maisha jela, lakini wataendelea kubaki kizuizini hadi Mei 22, 2024 kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo inayowakabili.

Taarifa ya Mahakama imewataja washtakiwa hao kuwa ni Dalerzdzhon Mirzoyev (32), Saidakrami Rachabalizoda (30), Shamsidin Fariduni (25) na Mukhammadsobir Faizov (19) na wawili kati yao walikiri kuhusika na shambulizi hilo.

Hata hivyo, watu hao walionesha dalili za kuwa hoi kwa kipigo, huku kukiwa na shaka kuhusu uhuru waliokuwa nao wakati wakijibu maswali waliyokuwa wakihojiwa.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAMBO YA KUZINGATIA KIJANA UNAPOTAKA KUOA.
Leo sina maneno mengi. Kijana Sasa umekuwa Mkubwa, imefikia hatua...
Read more
SABABU AL-HILAL OMDURMAN KUJIUNGA NA LIGI KUU...
MICHEZO Mkurungezi wa Bodi ya Ligi , Almas Kasongo amekiri...
Read more
West Ham secured 2-1 victory over Man...
In a captivating showdown on Sunday, West Ham turned up...
Read more
Manuel Ugarte (23) only arrived at Paris...
The Uruguayan began life at PSG brightly, featuring prominently under...
Read more
“Nigeria is happy”–Davido expresses joy in Nigeria...
New sensation taking over the internet of Davido’s wedding themed...
Read more
See also  DAVIDO VOICES SUPPORT FOR CUBANA CHIEF PRIEST AMID ALLEGED NAIRA ABUSE

Leave a Reply