WALIOFANYA SHAMBULIZI NCHINI URUSI WAKAMATWA WANNE

0:00

HABARI KUU

Serikali ya Urusi, imewafungulia mashtaka watu wanne wanaodaiwa kufanya shambulizi katika ukumbi wa Crocus City Hall jijini Moscow usiku wa kuamkia Machi 23, 2024 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 130 karibu na jiji la Moscow.

Watu hao wamefunguliwa mashtaka ya ugaidi katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny mjini Moscow ambapo huenda wakakabiliwa na hukumu ya maisha jela, lakini wataendelea kubaki kizuizini hadi Mei 22, 2024 kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo inayowakabili.

Taarifa ya Mahakama imewataja washtakiwa hao kuwa ni Dalerzdzhon Mirzoyev (32), Saidakrami Rachabalizoda (30), Shamsidin Fariduni (25) na Mukhammadsobir Faizov (19) na wawili kati yao walikiri kuhusika na shambulizi hilo.

Hata hivyo, watu hao walionesha dalili za kuwa hoi kwa kipigo, huku kukiwa na shaka kuhusu uhuru waliokuwa nao wakati wakijibu maswali waliyokuwa wakihojiwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

STAN BOWLES AFARIKI DUNIA
HABARI KUU Nyota wa zamani wa QPR, Manchester City na...
Read more
President Ruto Extends Olive Branch to Opposition,...
President William Ruto has unveiled the second batch of his...
Read more
PAPA ASHINDWA KUJIBU SWALI KUHUSU JAMII YA...
HABARI KUU. Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo...
Read more
WENYE MATATIZO YA MOYO KUKUMBWA NA MAGONJWA...
HABARI KUU Utafiti mpya wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete...
Read more
TANZANIA YAZINDUA MAGARI YA UMEME
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  TUNDU LISSU AMSHTUKIA MBOWE KUELEKEA 2025

Leave a Reply