WILLIAM RUTO KUMUIGA SAMIA KWENYE SOKA ATOA AHADI HIIDiscoverCars.com

0

0:00

MICHEZO

Rais William Ruto ameahidi kujitolea kufufua soka la Kenya katika kujenga miundombinu, maendeleo ya vijana na usaidizi kwa vilabu na timu za kitaifa.

Ameyasema hayo katika hafla ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 ya AFC Leopards huku Rais huyo akiahidi kutoa kitita cha milioni kumi kwa klabu hiyo.

Katika hotuba yake, Rais Ruto alikiri na kuvipongeza vilabu kama AFC Leopards, Gor Mahia, Bandari, na Shabana katika kukuza vipaji na kukuza maendeleo ya mpira wa miguu nchini humo.

Katika hafla hiyo Rais William Ruto aliambatana na baadhi ya watu mashuhuri, akiwemo Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri,Musalia Mudavadi, Waziri wa Michezo Ababu Namwamba, na Magavana kutoka Nairobi, Bungoma na Kisii.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Siri yafichuka kikao cha Pochettino na Todd Boehly
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading