HABARI KUU
Wanabari Wawili wa Mkoa wa Lindi wakiripotia Star TV& Radio Free Africa na mwingine wa Channel Ten wamefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Nyamwage mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani) usiku wa kuamkia Leo March 26 )
Sshuhuda wa ajali hiyo Alli Husein alisema Waandishi hao walikuwa wanatokea Dar es Saalam kwenye mafunzo kurejea mkoani Lindi.
Waandishi waliofariki dunia ni Abdalla Nanda wa Chanel Ten mkoa wa Lindi na Josephine Kibiriti wa Sahara Media Group (RFA na Star TV)
kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Rufiji (Pwani)Protasi Mutayoka amenukuliwa na Matukio Daima amethibitisha kutokea Kwa Ajali na kuwa Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 7 usiku wa March 26 na Chanzo ni Dereva wa “Kenta” ambaye baada ya ajali alikimbia na msako wa kumtafuta unaendelea.
Alisema kuwa kwenye gari ndogo ya waandishi walikuwa watu watatu na Wawili Mwanamke mmoja na mwanaume walifariki Dunia eneo la tukio na mmoja ni majeruhi amelazwa Hospitali na mguu wake mmoja amevunjika .
Kamanda huyo alisema eneo la ajali ni eneo zuri halina changamoto ya miundo Mbinu huku akitoa onyo Kwa madereva kufuata Sheria za usalama barabarani.