HABARI KUU
Mgombea Urais kutoka kambi ya upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ndiye Rais mpya wa Senegal baada ya kushinda Uchaguzi wa Rais nchini humo ikiwa ni wiki moja baada ya kutoka Gerezani.
Faye amechaguliwa kuwa Rais mteule wa taifa hilo akiwa na umri wa miaka 44 ambaye ataapishwa kuwa Rais wa Taifa hilo.
Rais huyo ameweka historia ya kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika na katika uchaguzi huo, maelfu ya Wasenegali walijitokeza katika maeneo mbalimbali wakisubiri kwa utulivu kupiga kura zao.
Abdoulaye Sylla, Msimamizi wa Tume ya Uchaguzi amesema idadi kubwa ya watu walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi huo.
Mgombea wa ushirika wa utawala nchini Senegal ambaye alikuwa mgombea mwenzake kwenye nafasi hiyo, Amadou Ba amempongeza mpinzani wake kutoka kambi ya upinzani, Faye kwa kushinda uchaguzi wa Rais.