PAUL MAKONDA AMTETEA MAGUFULI

0:00

HABARI KUU

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Paul Makonda, amewataka wale aliowaita Wanasiasa uchwara wanaojipendekeza kwa Rais Samia kwa kumtenganisha na Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kuacha mara moja tabia hiyo kwakuwa Viongozi hao wote ni kitu kimoja na hauwezi kuwatenganisha.

Akiongea Jijini Dar es salaam leo wakati wa mapokezi ya ndege mpya ya Air Tanzania, Makonda amesema “Mh. RC Chalamila hapa amenifurahisha kwelikweli, kuna kasumba ya ujinga unaoendelea wa kutaka kumtofautisha Dkt. Samia na Dkt. Magufuli, huwezi kuwatenganisha hao Watu na Viongozi wengi Wanafiki wanaotafuta kujipendekeza kwa Dkt. Samia kila wakipata jukwaa wanataka kumfanya kama Dkt. Samia sio sehemu ya Dkt. Magufuli”

“Kama Msemaji wa Chama (CCM) kila anachokifanya Dkt. Samia ndicho ambacho alikifanya Dkt. Magufuli na Watu hawa walisimama wakazunguka katika Taifa hili wakatafuta kura kwa pamoja huwezi kuwatenganisha na Waziri Mkuu wao yule pale Kassim Majaliwa, ningetamani leo iwe ni siku ya mwisho ya unafiki wa Viongozi na Wanasiasa uchwara wanaopambana kuwatenganisha Viongozi hawa, mafanikio haya tunayasherehekea wote kwasababu Chama ni kimoja, Serikali ni ya CCM na nyinyi Wananchi mliipigia kura”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

ATP roundup: Nicolas Jarry ousts home-country favorite...
Fifth seed Nicolas Jarry fended off a match point at...
Read more
MR IBU AFARIKI DUNIA
MICHEZO/BURUDANI Mchekeshaji na Mwigizaji Legend wa Nollywood Nigeria John Okafor maarufu...
Read more
Woman left in complete shock and heartbreak...
A Nigerian woman was shocked and saddened to learn that...
Read more
SABABU ZA DIAMOND PLATINUMZ KUKATAA SHOW ZA...
NYOTA WETU
See also  BITEKO AZUIA LIKIZO ZA WAFANYAKAZI WA TANESCO
Diamond Platnumz amesema shoo za Nigeria anazikataa mara...
Read more
UCHAMBUZI WA VYEO KATIKA JESHI LA POLISI...
MAKALA Hakuna cheo kinachoitwa RPC wala OCD wala OCS katika...
Read more

Leave a Reply