HABARI KUU
Rais wa Urusi Vladmir Putin amekiri kwa mara ya kwanza kuwa watu itikadi kali ndio waliohusika na shambulizi la wiki iliyopita kwenye ukumbi wa tamasha la muziki nje ya mji Mkuu Moscow.
Putin ameyasema hayo katika mkutano uliorushwa mubashara kwenye luninga, akisema wanafahamu uhalifu huo ulifanywa na watu wa misimamo mikali, ambao itikadi yao imekuwa ikipingwa na ulimwengu wa Kiislamu kwa karne nyingi.
Amesema, maswali mengi bado hayajajibiwa ikiwa ni pamoja na ni kwa nini washambuliaji hao walijaribu kukimbilia Ukraine madai ambao Kyiv iliyapinga.
Putin ameongeza kuwa, uhalifu huo huenda ukawa kiunganishi katika mfululizo mzima wa majaribio ya wale ambao wamekuwa katika vita na Urusi tangu mwaka wa 2014.
Watu 11 walikamatwa kuhusiana na shambulio hilo lililotokea katika jengo la Crocus City Hall, ambapo walivamia na kuwafyatulia risasi washiriki wa tamasha la muziki kabla ya kulichoma moto jengo hilo na kuwauwa karibu watu 139 an wengine 180 kujeruhiwa.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.