DARAJA LA FRANCIS SCOTT KEY LAUA WATU 6

0:00

HABARI KUU

Sita wahofiwa kufa tukio la daraja kuporomoka Marekani

Huku shughuli ya kuwatafuta ikiendelea wafanyakazi sita waliotoweka baada ya Daraja la Francis Scott Key mjini Baltimore, Marekani kuporomoka jana Jumanne wanahofiwa kuwa wamefariki dunia.

Mkuu wa polisi wa Jimbo la Maryland Roland L. Butler Jr., amesema Jumanne jioni kuwa operesheni ya utafutaji na uokozi sasa inabadilishwa kuwa ya utafutaji wa miili.

Amesema wapiga mbizi watarejea katika eneo la tukio asubuhi (kwa saa za Marekani) kwani mazingira ya usiku yalikuwa magumu kidogo kwao.

Meli kubwa ya shehena iligonga nguzo ya daraja hilo na kusababisha kuvunjika vipandevipande na kutumbukia majini.

Gavana wa Maryland amesema wahudumu wa meli hiyo walituma ujumbe wa dharura wa kuomba msaada muda mfupi kabla ya tukio hilo kutokea, hatua iliyowasaidia maofisa kupunguza idadi ya magari kwenye daraja hilo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

RAIS JAVIER MILEI KUWAFUTA KAZI WAFANYAKAZI WA...
HABARI KUU Rais Javier Milei amepanga kuwafuta kazi Wafanyakazi wa...
Read more
Enzo Fernandez has apologised to several French...
The Argentina international, 23, landed in Atlanta in the United...
Read more
SEVEN SUGGESTIONS ON RENEWING FEELINGS IN THE...
LOVE ❤ ✔️People can lose feelings for their partners for...
Read more
SABABU MARIOO KUFUNGULIWA KESI
NYOTA WETU Msanii Toto Bad maarufu kama @marioo_tz amefunguliwa kesi...
Read more
WHY MEN DELAY GETTING MARRIED
1) FEAR (MARRIAGE PHOBIA) Many bachelors actually fear Marriage They fear the...
Read more
See also  WANANCHI WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI MKOANI NJOMBE ILI KUDHIBITI UHALIFU

Leave a Reply