FC BARCELONA KUMUUZA ANSU FATI

0:00

MICHEZO

Klabu Bingwa nchini Hispania FC Barcelona imesema inatarajia kumuuza mchezaji wake Ansu Fati mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anayekipiga kwa mkopo katika timu ya Brighton ya nchini England, atauzwa mwishoni mwa msimu huu kwenda timu watakayofikia mwafaka.

Taarifa iliyotolewa katika mtandao wa klabu ya Barcelona, ilisema kuwa wanatarajia kumuuza mchezaji huyo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa hiyo ilisema watamuuza Ansu Fati baada ya baadhi ya timu kuonyesha nia ya kuitaka saini yake.

Imeeongeza kuwa, waliamua kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo kwenda Brighton kuhakikisha anaongeza kiwango chake tangu mwaka jana.

“Tulimtoa fati kwa mkopo kwenda Brighton lakini ameshindwa kupanda kiwango, hivyo tumefikia mwafaka wa kumuuza mwishoni mwa msimu huu,” ilisema taarifa hiyo.

Fati amecheza mechi 15 katika kikosi cha Brighton na kufanikiwa kufunga mabao mawili pekee.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Manchester United wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe...
Mabao ya kipindi cha kwanza kutoka kwa Alejandro Garnacho na...
Read more
WHY MEN NEED TO LEARN ABOUT WOMEN
Women fall in love with words. Words communicate your intentions...
Read more
KAULI YA MAKONDA YAZUA KIZAAZAA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Viwango vya bei za mafuta vyashuka
Bei ya mafuta nchini kwa mwezi Juni imeshuka ambapo katika...
Read more
KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?
Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye...
Read more
See also  MOURINHO AANZA VITA YA MANENO NA GUARDIOLA

Leave a Reply