Polisi wa Argentina wanachunguza vitisho vya kifo vilivyotolewa kwa familia ya mshambuliaji Angel Di Maria nyumbani kwao Roasario.

0:00

Wafanyakazi kwenye nyumba ya staa huyo mshindi wa Kombe la Dunia na Argentina mwaka 2022, walisema walikutana na ujumbe uliokuwa na vitisho vya vifo kama ataendelea kucheza kwenye moja ya klabu katika mji wa Rosario.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 36 anayecheza Benfica ya Ureno hivi karibuni alisema anaweza kurejea kucheza kwenye klabu yake ya utoto ya Rosario Central. Kwa sasa yuko Marekani na timu ya taifa ya Argentina.

“Vitisho kama hivi vinasababisha usumbufu mwingi kwenye jamii na hilo ndio lengo lake, kufanya wananchi wawe na hofu, kuwatisha watu muhimu kwenye jamii,” alisema Esteban Santantino, anayefanya kazi kwenye vyombo vya usalama katika mji wa Rosario.

Vyombo vya habari vinasema malengo ya vitisho hivyo bado hayako wazi, ingawa Polisi walishindwa kukataa taarifa zozote za uchunguzi.

Di Maria alianza kwenye mchezo wa jana wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Costa Rica kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo, Lionel Scaloni.

“Di Maria anafahamu tuko nyuma yake kwa chochote atakachohitaji. Kitu muhimu ni kwamba alicheza, hicho kitamfanya apate faraja kidogo.

Rosario imekumbwa na matukio ya vurugu nyingi miongoni mwa magenge yanayohusika na uuzaji wa dawa za kulevya. Mauaji ya watu kwenye mji huo ni watu 22 kwa 100,000.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SENDIGA AZINDUA OFISI YA WAMACHINGA NA BODABODA
HABARI KUU Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amezindua...
Read more
KIZIMBANI KWA MASHTAKA YA KUMWINGILIA MBUZI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MANCHESTER UNITED KUIKOSA UEFA
MICHEZO
See also  How To Grow Your Small Business
Huenda Manchester United wakashindwa kushiriki kwenye michuano ya ligi ya...
Read more
3 THINGS YOU NEED TO DO TO...
1) HAVE STANDARDS From dozens of practical counseling sessions I've done...
Read more
WAWILI WASHIKILIWA NA POLISI KISA KUUZA INTANETI
HABARI KUU Jeshi la Polisi Kanda Maalum linawashikilia Claudian...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply