HABARI KUU
Mwanaume Mkazi wa Kitelewasi Mkoani Iringa aitwae Dickson Mbwilo (42), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti Mke wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa SACP Allan Bukumbi amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa akimfanyia Mke wake kitendo hicho kama sehemu ya adhabu pale anapomkosea.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye jina lake limehifadhiwa, alikiri ni kweli Mumewe alikuwa akimfanyia kitendo hicho kila alipokuwa amekosea hali ambayo ilimpelekea kusababisha sehemu za siri kuharibika vibaya.
Katika hukumu nyingine, Watu wengine wawili Kheri Lutumo (25) wa Malangali Wilayani Mufindi na Mathayo Kitosi (34) wa Isele Wilayani Kilolo Mkoani Iringa, wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka Watoto wenye umri wa miaka 8 ambao walikuwa wakisoma darasa la pili.