MALAM BACAI SANHA JR AHUKUMIWA MIAKA 6 JELA KWA KUSAFIRISHA DAWA ZA KULEVYA

0:00

HABARI KUU

Mahakama nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha zaidi ya miaka sita mtoto wa Rais wa zamani wa Guinea-Bissau Malam Bacai Sanha Jr almaarufu kama ”Bacaizinho” kwa makosa ya usafirishaji wa Kimataifa wa dawa za kulevya.

Sanha Jr (52), ni mtoto wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Malam Bacai Sanha, aliyeongoza kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2012 alipofariki.

Sanha Jr anahusishwa na Mapinduzi yaliyofeli Februari 2022. Alikabidhiwa kwa Serikali ya Marekani Agosti 2022 baada ya kukamatwa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa FBI,

”Sanha Jr alikuwa akisafirisha dawa kwa nia ya kupata pesa za kufadhili mapinduzi yatakayomuwezesha kuwa Rais wa Guinea-Bissau ambapo walipanga kuanzisha utawala wa dawa za kulevya”.

Amewahi kushikilia nafasi mbalimbali katika Serikali ikiwemo ya mshauri wa masuala ya Uchumi wa baba yake wakati alipokuwa Rais.

Guinea-Bissau ni kitovu maarufu cha biashara haramu ya dawa za kulevya. Ni njia kuu inayotumika kusafirisha dawa hizo kutokea Amerika Kusini kwenda Ulaya.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Yankees heartbroken after 'cruel' World Series defeat
NEW YORK, - The New York Yankees' first trip to...
Read more
Former Super Eagles team player Dimeji Lawal...
Nigerian forward Victor Osimhen is currently making waves at Napoli,...
Read more
Focused Fritz outlasts Zverev to reach ATP...
TURIN, Italy, 🇮🇹 - Taylor Fritz became the first American...
Read more
FACTS ABOUT SLEEP SEX AND INTIMACY
❤ 1. When you go to bed clean and not...
Read more
'Milan suffered together' in gritty win against...
AC Milan manager Paulo Fonseca praised his team's resilience in...
Read more
See also  MUSEVENI AIAGIZA WIZARA KUCHUNGUZA MALI ZA SPIKA ANITA AMONG

Leave a Reply