SAKATA LA MBUNGE OLE-SENDEKA KUSHAMBULIWA LIKO HIVI

0:00

HABARI KUU

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, DCP David Misime amesema Polisi wanafuatilia tukio la kufyatuliwa risasi kwa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka na Dereva wake wakati wakiwa safarini tukio lililotokea katika Kijiji cha Ngabolo kilichopo Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

Misime ameyasema hayo na kuongeza kuwa wanafuatilia tukio hilo kwa ukaribu na uchunguzi ulishaanza mara tu baada ya kupokea taarifa.

Amesema,

“Timu ya Wataalamu wa uchunguzi wa matukio na matumizi ya risasi kutoka Makao Makuu ya Polisi Dodoma imetumwa kwenda kushirikiana na Timu ya Mkoa wa Manyara kuchunguza tukio hilo.”

“Ushirikiano huo unalenga kubaini waliohusika ni akina nani na madhumuni au kusudio lao lilikuwa ni nini na baada ya uchunguzi wa Wataalamu taarifa kamili itatolewa,”

amesema DCP Misime.

Katika tukio hilo, watu wasiojulikana walimfyatulia risasi zisizopungua nne Mbunge huyo wa Simanjiro akiwa ndani ya gari lake sna Dereva wake majira ya saa moja usiku Machi 29, 2024 na kisha kukimbia muda mfupi baada ya Mbunge huyo naye kuanza kupiga risasi juu kuwatishia.

“Ni kweli nimeshambuliwa kwa risasi majira ya saa moja kasoro katika Wilaya ya Kiteto kati ya Kijiji cha Ngabolo na Ndedo, kulikuwa na gari ambayo ilikuwa inanifuatilia kwa nyuma tukawapisha kidogo kama tunataka kuwapisha wapite kulia walipofika usawa wetu wakaanza kumimina risasi kwa Dereva na baada ya hapo wakavuta kwenda mbele halafu wakaanza kuzipiga za usoni na sisi tukakata kona kugeuza na Mimi nikaanza kupigapiga (risasi) za juu pale kuwatishiatishia ndio tukafanikiwa kugeuza na kuondoka.”

alisimulia Ole Sendeka.

Amesema,

“walikua na silaha kubwa na silaha ndogo, hakuna aliyepata madhara tulikuwa Mimi na Dereva wangu ni gari tu ndio wameichakazachakaza wameipigapiga, mpaka sasa kwakuwa tumekuja gizani huku hatujazihesabu lakini zipo risasi moja, mbili, tatu, nne kama nne hivi hatujazihesabu.”

See also  FREEMAN MBOWE ATAKA TANGANYIKA ITAMBULIKE KAMA ILIVYO ZANZIBAR
Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAMBO 20 YA KUZINGATIA KWA ALIYE NA...
MASTORI 1. JENGA MAKAZI YAKO MAPEMA. Iwe ni mjini au...
Read more
How to keep cows for dairy production.
To keep cows for dairy production, you will need to...
Read more
Sababu za Ukosefu wa Nguvu za kiume...
Upungufu wa nguvu za kiume ni hali ya kushindwa kufanya...
Read more
ISLAMIC STATE YAHUSIKA KWENYE VIFO VYA WATU...
HABARI KUU Idadi ya watu waliokufa kwenye shambulizi la la...
Read more
Acting Police IG Vows Tight Security for...
Acting Police Inspector General (IG) Gilbert Masengeli has emphasized the...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

This Post Has 2 Comments

  1. Hello

    I have just verified your SEO on juniitv.online for its SEO metrics and saw that your website could use an upgrade.

    We will improve your ranks organically and safely, using only state of the art AI and whitehat methods, while providing monthly reports and outstanding support.

    More info:
    https://www.digital-x-press.com/unbeatable-seo/

    Regards
    Mike Nicholson

    Digital X SEO Experts

Leave a Reply