HABARI KUU.
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Deogratias Ndejembi kuwa Waziri wa Kazi, Ajira Vijana na Wenye Ulemavu, akichukua nafasi ya Profesa Joyce Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Kabla ya uteuzi huo, Ndejembi alikuwa Naibu Waziri wa Tamisemi.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Zainab Katimba kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, akichukua nafasi ya Deogratius Ndejembi ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu).
Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Dk Edwin Mhede kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uvuvi na Mifugo.
Kabla ya uteuzi huo, Dk Mhede alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mabasi Yaendayo Kasi (DART).
Uteuzi wa Dk Mhede, unachukua nafasi ya Agnes Meena, ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Daniel Baran Sillo, ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya Jumanne Sagini ambaye amehamishiwa Wizara ya Katiba.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dk Suleiman Serera kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kabla ya uteuzi huo, Dk Serera alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Rais Samia Suluhu Hassan,amemteua Maryprisca Mahundi kuwa Naibu Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
kabla ya uteuzi huo, Mahundi alikuwa Naibu Waziri wa Maji.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Saidi Mtanda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akichukua nafasi ya Amoss Makalla. Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Makalla atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Mtanda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kabla ya uteuzi huo, Makonda alikuwa Katibu wa Uenezi, Itikadi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM).