NYOTA WETU
Rapa wa Marekani Yung Miami anatuhumiwa kwa kumbebea Diddy dawa za kulevya aina ya “Pink Cocaine” au “Tuci”. Hii ni Kwa Mujibu Wa Nyaraka Mpya za Kisheria Katika Kesi Iliyofunguliwa Na Mtayarishaji Rodney Jones Dhidi ya Diddy
Katika kesi hii Rodney anadai kuwa Yung Miami alimbebea Diddy dawa za Kulevya Kwenye Ndege Binafsi Kutoka Miami Hadi Virginia Wakati Diddy akiwa Kwenye Mazoezi (Rehearsal) Ya Tamasha La ‘Something In The Water’ Lililofanyika 2023.
Rodney amedai Kwamba; ‘Punda’ au Mbeba Madawa Ya Kulevya Wa Diddy ‘Brendan Paul’ Alisahau Kubeba Dawa Hizo, Ndipo Brendan Alipompigia Simu Yung Miami Na Kumpa Jukumu La Kusafirisha Mzigo Huo Wa ‘Cocaine’ KwaAjili Ya Diddy Ambaye Alionekana Kutokuwa Sawa.
Kumbuka Rodney Jones ni Miongoni mwa wahanga Katika Kesi za Unyanyasaji Wa Kingono Za Diddy Ambapo Yeye Alimfungulia Mashtaka Diddy Akidai Tsh Bilioni 76.5 Kwa Kufanyiwa Ukatili Kama Kushikwa Maumbile Yake, Kufanya Ngono Na Wanawake Wanaojiuza, kulazimishwa Kutumia Dawa Za Kulevya Lakini Pia kudhulumiwa malipo ya uandaaji Wa ‘The Love Album: Off the Grid’ Iliyotoka Mwaka Jana. Sio Hivyo Tu Jones Anadai Pia Diddy Alimuahidi Atampa Tuzo Na Kumfanya Awe Maarufu Na Kumtafutia Kazi Kwenye Kampuni Kubwa Za Biashara Za Muziki.
Hata Hivyo wanasheria wa Diddy walidai kuwa Jones alitunga kashfa Hizo kwa lengo la Kujipatia Fedha.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.