AZIZ KI AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU YA TANZANIA BARA

MICHEZO

Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Aziz Ki ameteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu msimu wa 2023/2024, huku Bruno Ferry wa klabu ya Azam, akichaguliwa Kocha Bora wa ligi hiyo kwa mwezi huo.

Ki amewashinda Feisal Salum wa Azam na Clatous Chama wa klabu ya Simba Sc alioingia nao fainali kwenye mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF).

Kwa mwezi Machi, Ki alionesha kiwango kikubwa na kuisaidia time yake kupata ushindi katika michezo mitatu kati ya minne ambayo Young Africans ilicheza, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao matatu na kuhusika na mengine matatu, hivyo kuwawezesha Wananchi kukusanya alama tisa na kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Young Africans iliifunga Ihefu mabao 5-0, ikaifunga Geita Gold bao 1-0, ikaifunga Namungo mabao 3-1 na ilipoteza mabao 2-1 dhidi ya Azam. Ki alicheza jumla ya dakika 330 za michezo hiyo.

Kwa upande wa Bruno aliiongoza Azam FC kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kuendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Azam FC iliifunga Young Africans mabao 2-1, iliifunga Dodoma Jiji mabao 4-1 kisha ikatoka sane ya bao moja na Coastal Union.

Bruno amewashinda Miguel Gamondi wa Young Africans na Zuberi Katwila wa Mtibwa Sugar alioingia nao fainali.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Shabani Rajabu kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Machi, kutokana na kufanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu uwanjani.

See also  Milan's Fonseca praises substitutes after Brugge win

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

SANJAY DUTT ATUA NCHINI KUFANYA ROYAL TOUR...
Michezo Msanii maarufu Duniani kwenye eneo la filamu kutoka nchini...
Read more
Mayorkun claims to have no familiarity with...
CELEBRITIES Musician Mayorkun, claims to have no familiarity with Nicki...
Read more
There was no "Miracle on the Seine"...
With the French sporting spotlight locked on the Bercy Arena,...
Read more

Leave a Reply