BASSIROU DIOMAYE FAYE AAPISHWA RASMI KUWA RAIS WA SENEGAL

0:00

NYOTA WETU

Mwanasiasa wa mrengo wa kushoto, Bassirou Diomaye Faye, ameapishwa hii leo kuwa rais wa tano wa Senegal na kuahidi mabadiliko ya kimfumo, uhuru na utulivu baada ya miaka kadhaa ya machafuko.

Sherehe za kuapishwa kwake zimefanyika katika mji mpya wa Diamniadio, karibu na mji mkuu Dakar.

Faye mwenye umri wa miaka 44, ambaye anakuwa rais kijana zaidi kuwahi kuliongoza taifa hilo la Afrika Magharibi, amekula kiapo mbele maafisa wa Senegal pamoja na wakuu wa nchi kadhaa za Kiafrika.

Faye analenga kuibadilisha Senegal kiuchumi kwa kutumia gesi na mafuta.
Katika hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi, Faye ambaye ni mshirika mkuu wa kiongozi maarufu wa upinzani, Ousmane Sonko, alisema vipaumbele vyake ni maridhiano ya kitaifa, kukabiliana na kupanda kwa gharama ya maisha na kupambana na ufisadi.

Lakini changamoto kubwa inayomkabili itakua kukabiliana na viwango vya ukosefu wa ajira,hasa kwa vijana ambao ni karibu asilimia 75 katika nchi yenye watu milioni 18.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Challenges facing Onion Farming
Rains or Excess Watering:Too much rains or excess watering can...
Read more
Brad Gilbert announces end of Coaching Relationship...
World No. 6 Coco Gauff and coach Brad Gilbert are...
Read more
Fat Joe amtaja 50 Cent Kuwa Rapa...
Rapper wa Unyamwezini Marekani ‘Joseph Antonio Cartagena’ a.k.a ‘Fat Joe’,...
Read more
Roma coach Ivan Juric relieves pressure with...
ROME — Roma coach Ivan Juric may have saved his...
Read more
5 THINGS MORE VALUABLE THAN A WOMAN'S...
Dear Bachelor,If the major Reason you are marrying a lady...
Read more

Leave a Reply