MAPIGO 10 YA CCM KWA MZEE EDWARD LOWASSA ALIYOPITIA BAADA YA KUJIUNGA NA CHADEMA

0:00

MASTORI

MAPIGO 10 YA CCM KWA MZEE LOWASSA.

Haikuwa Jambo rahisi kwa CCM kumshuhudia Kiongozi mkubwa ngazi (Waziri Mkuu) kukihama CCM na kujiunga na Chama cha upinzani CHADEMA.

Usiwaone leo CCM msibani wanalia na kupishana kutoa maneno mazuri kwa Mzee Lowassa ukajua hadi roho zao ni nzuri, HAPANA.

Ukiondoa vicheko, tabasamu na maneno matamu ya CCM wanapokuwa mbele ya kamera huwa wanaupande wa pili wa sura zao na roho zao.

Lowassa alishawahi kuziona sura halisi za CCM, tena waliokuwa Viongozi wenzie, marafiki,’family friends’ na aliokuwa anakula na kunywa nao kila siku. Baada ya kugusa maslahi yao kwa kuihama CCM

Walimpiga mapigo haya

1. Pigo la kwanza,ilikuwa marafiki aliokuwa nao katika kambi yake ya CCM (safari ya matumaini) na waliomshawishi ‘amwage mboga’ kwa kuihama CCM.Baada ya Lowassa kutii ushauri wao.marafiki hao hawakuhama,wakabakia CCM.

2. Baada ya uchaguzi 2015,Serikali ya CCM ikamuondoa mtoto wa kike wa Lowassa ( Pamela ) aliyekuwa anafanya kazi BOT Makao makuu Dar es Salaam na kumpeleka BoT tawi la Arusha tena bila kupangiwa kazi yoyote.

3.Apiri 16,2016 Mkwe wa Edward Ngoyai Lowassa (Sioi Sumari) akafunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha $6M akakaa gerezani miaka.

4.Haikutosha,Shamba la kufugia na kukuzia mifugo la Mzee Edward Ngoyai Lowassa lililopo Mkoani Tanga,Handeni likakatwa kuporwa na serikali lote,Waziri mmoja kutoka Baraza la mawaziri la Magufuli akashauri walimege nusu tu,badala ya kupora lote. Wakalichukua nusu.

4. Shamba lingine la Mzee Lowassa lilipo mkoani Tanga ,Loshoto likiwa linasafishwa na Bulldozer, Serikali wakazuia zoezi lisiendelee. wakampelekea Mzee Lowassa bill ya billion 10,kama malimbilizo ya kodi ya ardhi ya shamba lile.Mzee akalitema,Serikali wakalibeba.

5.Serikali ya CCM,pia wakamfuata Fred Lowassa (mtoto wa Kiume wa kwanza wa Mzee Lowassa) wakamlima kodi kupitia TRA kiasi cha zaidi ya Tsh billioni 5,katika biashara zake,wakazifunga akaunti zake binafsi na za biashara mpaka atakapolipa kodi zote.

6.Mzee Lowassa alikuwa anatibiwa na kuhudumiwa na Serikalini,kama Waziri Mkuu Mstaafu,ambapo alikuwa anaenda katika klinic ya matibabu nje ya nchi kila mwaka.

Lakini baada ya kuhamia CHADEMA wakafuta huduma hiyo Mzee Lowassa akawa anajihudumia mwenyewe kwa fedha zake katika matibabu.

7. Mzee Lowassa alikuwa anaishi Dodoma maeneo ya Area D,katika nyumba za Serikali (TBA) Kama mpangaji na Mtanzania mwingine

(Ile nyumba ambayo alipokuwa CCM watu mbalimbali walikuwa wanaenda kumuomba agombee urais)

aliporwa ile nyumba na serikali ya CCM,kwa sasa nyumba ile amepewa Rais Hussein Mwinyi anaitumia kama makazi yake anapokuwa Dodoma.

8.Pigo jingine,mlinzi wa muda mrefu wa Mzee Lowassa Bw. Tendewa ambaye alikuwa siyo mlinzi tu bali mtu wa karibu kwa miaka mingi sana,
alisimamishwa kazi punde baada ya Mzee Lowassa kuhamia CHADEMA tu akiwa amebakisha miezi 6 kustaafu utumishi wake,na akapoteza mafao yake yote.

9.Wafanyabiashara na marafiki wa Mzee Lowassa Dar na Arusha wakafilisiwa,wengine kutishwa mashitaka au kufuatiliwa na TISS kama bado wanamawasiliano na Lowassa (wakataka afe njaa)

10.MONDULI-Siku moja Serikali ilienda Mkoani Arusha,Monduli katika shamba la Mwekezaji (Mzungu) wakiamini ni Shamba la Mzee Lowassa wakalitaifisha na kisha wakaligawa kwa Wanakijiji kumkomoa Mzee Lowassa.
lakini halikuwa shamba lake bali la Mwekezaji wa miaka mingi.

Wakahakikisha pale Monduli wanaondoa heshima ya Mzee Lowassa kwa kuweka DC atakayekuwa anamdhalilisha Mzee Lowassa
wakahamisha Mbunge na Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Monduli kutoka CHADEMA kuhamia CCM ili kufuta kabisa usuli(legacy) ya Mzee Lowassa.

Mwisho
Mapigo yote haya hayakumfanya Mzee Lowassa Kupiga magoti kwa serikali ya CCM au kurudi CCM.

kwa muda wa miaka 4,kuanzia 28-07-2015 alipohamia CHADEMA hadi tarehe 28 -02- 2019 alikuwa ni mtu mwenye msimamo mkali sana usiotetereka.

01/03/2019 Lowassa alirudi CCM ili kumnusuru rafiki yake kipenzi ROSTAM AZIZI ambaye alipigwa mapigo mawili tu na serikali ya CCM.

See also  SABABU ZA MASHABIKI KUWATUPIA PESA WACHEZAJI WA NEWCASTLE

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mbwana Samatta aisaidia PAOK kubeba Ubingwa
MICHEZO Nahodha wa kikosi cha Timu ya Taifa Tanzania (Taifa...
Read more
Mohbar's wife Wunmi ,is said to have...
CELEBRITIES Investigative journalist Stella Dimokokorkus reports that Wunmi, the late...
Read more
DJ Cuppy made headlines as she reacts...
The vibrant Nigerian disc jockey and billionaire heiress, Otedola Florence...
Read more
Leicester City will be without injured forward...
The 25-year-old Zambia striker has undergone surgery after suffering an...
Read more
SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA
MAKALA SHULE KUMI GHALI ZAIDI TANZANIA.International School of Tanganyika (IST)—...
Read more

Leave a Reply