0:00

HABARI KUU

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma limetoa taarifa ya hitilafu ya kivuko cha abiria MV Malagarasi kinachofanya shughuli ya kuvusha abiria na mizigo mto Malagarasi eneo la llagala, Wilayani Uvinza ambapo muda wa saa 10:30 Asubuhi kikiwa kinavusha abiria injini za kivuko hicho zilizima ghafla kupelekea kusombwa na maji na kuzua taharuki kwa abiria.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, SACP Filemon K. Makungu imebainisha kuwa jitihada za kuokoa abiria na mizigo zimefanyika kwa ushirikiano baina ya vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi, hakuna madhara yeyote yaliyojitokeza kwa abiria na mizigo.

ā€œAdha, mafundi wamefanikiwa kufanya matengenezo ya injini hizo kisha kivuko hicho kurejea eneo la maegesho.ā€

ā€œJeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma linatoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuwa watulivu na kuondoa hofu badala yake waendelea kutekeleza majukumu yao ya kujiletea maendeleo.ā€

imesema taarifa hiyo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  MPINZANI NCHINI CHAD ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading