MAKALA
Kwenye mpira wa miguu,mastaa wa kike wa Tanzania nao hawako nyuma kuupenda na kuunga mkono mchezo huu. Hii ni orodha ya baadhi ya mastaa wanaoshabikia timu za Simba na Yanga.
Hamisa Mobetto – Simba
Msanii wa filamu, mziki, mjasiriamali na mmoja ya wanawake wenye wafuasi wengi mtandao wa Instagram 10.2 Milioni Hamisa Mobetto ni shabiki mkubwa wa Klabu ya Simba.
Alianza kuipenda Simba wakati Haji Manara anawatumikia wekundu hao wa Msimbazi, na siku yake ya kwanza kwenda uwanjani unaambiwa alikua hajui chochote na kuuliza kila kinachoendelea Uwanjani.
Zuchu – Simba
Kutoka hapo lebo ya WCB bi dada Zuhura naye ni mnyama unakumbuka alichokifanya siku ya Simba Day mwaka 2022 kwa Mkapa.
Aliibuka na bonge moja la Surprise kwa kushuka na kamba kutoka juu ya uwanja huo kama Mjeshi akisema Simba mashabiki wanaitikia nguvu moja na kufanya bonge moja la show.
Salama – Simba
Salama na Simba ni damdam bila kuficha chochote huwa anaonesha mahaba yake ya wazi wazi kwa mnyama Simba.
Ni mtangazaji na producer lakini ni shabiki mkubwa wa mchezo huu wa soka timu yake ni Simba na Man United na ukipitia kwenye page yake ya Instagram utaona anapost wachezaji kama Mbwana Samatta, Baleke, Chama, Fei Toto, Messi, Mbappe na Varane.
Wema Sepetu – Yanga
Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu ni staa wa kike anayeongoza kuwa na wafuasi wengi mtandao wa Instagram ana followers Milioni 10.5 pia ni mwananchi wa kijani na njano haswa.
Unakumbuka ukaribu wake na aliyekuwa mchezaji wa Yanga Carlinhos alivyozua gumzo baada ya kusambaa kwa picha zao mitandaoni kabla ya mchezaji huyo kutimkia nchini kwao Angola.
Nandy – Yanga
The African Princess Nandy naye ni mwananchi kabisa tena yeye na Mume wake Billnass wote ni mashabiki ya Yanga.
Ikumbukwe ameshatoa mpaka ngoma kuhusu Yanga na alifanya show ya kufa mtu siku ya kile cha siku ya Mwananachi kwa Mkapa 2021.
Shilole – Yanga
Mpishi na msanii wa mziki Shishi Baby Shilole ni shabiki mkubwa wa Klabu ya Yanga, mapenzi yake kwa timu hiyo hayajifichi kwani ikifanya vizuri huwa anashea hisia zake kwa kuandika kwenye mtandao wake wa Instagram.