HABARI KUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Mbio za Mwenge mwaka huu zitaendelea kutoa hamasa kwa jamii kusitisha biashara na matumizi ya dawa za kulevya kwani bangi na mirungi zimeendelea kutumika kwa wingi.
Amesema vijana wamekuwa wakitumia aina nyingine ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi inayofahamika kama ‘Cha Arusha’ na ‘Skanka’.
Akizungumza leo Aprili 02 wakati akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2024 mkoani Kilimanjaro, Majaliwa ametoa wito kwa vijana kuacha kutumia dawa hizo za kulevya akisema dawa hizo, Cha Arusha na Skanka zinawafanya kuwa vichaa.
Aidha Majaliwa amesema Mbio za Mwenge mwaka huu zitaendelea kutoa hamasa kwa jamii kusitisha kilimo haramu cha bangi na mirungi pamoja na kusitisha biashara na matumizi ya dawa za kulevya.