NYOTA WETU
Mtu Mzee kuliko wote duniani (kati ya waliopo kwenye rekodi rasmi) Juan Vicente Perez (114), amefariki dunia, ikiwa ni miezi miwili kabla hajatimiza miaka 115.
Mzee Perez kutokea Venezuela alithibitishwa kuwa mtu mzee kuliko watu wote na rekodi za Guiness World wakati akiwa na umri wa miaka 112.
Mzee huyo alisema kuishi kwake kwa muda mrefu kulitokana na kufanya kazi kwa bidi, mapumziko, kuwahi kulala, kunywa glasi 1 ya kinywaji kikali kila siku, kumpenda Mungu na kumbeba moyoni mwake kila wakati.
Perez alizaliwa Mei 27 mwaka 1909, alimuoa Edofina del Rosario Garcia na ndoa yao ilidumu kwa miaka 60 hadi bibi huyo alipofariki dunia mwaka 1997.
Perez na mke wake walijaaliwa kupata watoto 11, wajukuu 42 , vitukuu 18 pamoja na vilembwe 12.