HABARI KUU
“Mimi niliona ni goli”
Akizungumza na Idhaa ya Taifa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt . Tulia Akson Mwansasu ametoa maoni yake kuhusu goli lililofungwa na Yanga.
“Niseme kama Mtanzania ningetaraji timu zetu zingesonga zaidi ila wamejitahidi kwa kweli kufika robo fainali timu mbili kutoka nchi moja sio jambo dogo. Kwa sababu sizijui sana sheria za mpira wa miguu lakini kwa sababu mpira ulidunda ndani ya ule mstari ningefikiri ni goli ni sawa na mpira ungepiga mwamba ukaingia ndani halafu ukatoka ningesema ni goli lakini sasa wale wataalamu wamesema sio goli nafikiri tukubaliane nao lakini lilipoingia tu nikasema ni goli,”
amesema Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson
Dkt. Tulia amesema hayo wakati wa mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kuhusu Bunge Marathon litakalofanyika Aprili 13, 2024 katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.