HABARI KUU
Muungano wa wafanyakazi wa mafuta nchini Nigeria umemuomba Rais Bola Tinubu kupeleka wanajeshi zaidi, ili kukabiliana na wizi wa mafuta.
Ombi hilo linakuja kufuatia wizi mkubwa wa mafuta kwenye mabomba na visima ambao umekuwa ni changamoto kwa Tinubu katika miaka ya hivi karibuni, huku ikidaiwa anapoteza fedha za Serikali na kupunguza pato na mauzo nje ya nchi.
Nigeria ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika, na anategemea bidhaa hiyo kwa zaidi ya theluthi mbili ya mapato yake na takriban asilimia 90 ya mapato ya fedha za kigeni.
Hata hivyo inadaiwa kuwa pato la mafuta lilifikia mapipa milioni 1.48 kwa siku mwezi Februari, ingawa uzalishaji wa mafuta unaimarika hatua kwa hatua, lakinj bado uko chini ya lengo la bajeti la mapipa milioni 1.78 kwa siku.