HABARI KUU
Siku tatu baada ya kuapishwa kwa Rais wa tano wa nchi ya Senegal Bassirou Diomaye Faye, Waziri Mkuu Ousmane Sonko ameunda Serikali mpya yenye Mawaziri 25 na Makatibu watano wa Serikali.
Katika Mawaziri hao ishirini na tano, karibu kumi kati yao walikuwa wanaunda serikali iliyopita chini ya Macky Sall.
Waziri wa Mambo ya Nje ameteuliwa Yassine Fall huku katika Wizara ya Nishati akiteuliwa Mwanamke.
Watendaji 13 kutoka katika Chama cha kisiasa cha Pastef wamewekwa katika nyadhifa zote za Mawaziri kama vile El Malick Ndiaye, aliyeteuliwa katika Wizara ya Miundombinu na Uchukuzi na Msemaji wa Serikali na Amadou Moustapha Ndiak Saré akiteuliwa kuwa Waziri wa Mafunzo ya ufundi.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.