MICHEZO
Kwa mara ya kwanza Mwamuzi wa kati aliyechezesha mechi ya juzi kati ya Mamelodi Sundowns na Yanga Beida Dahane raia wa Mauritania amefunguka kwamba asilaumiwe kwa lolote lile kwenye sakata la goli la Aziz Ki kukataliwa bali lawama zote ziwaendee waliokuwa wana-control Video Assistant Referee (VAR).
Mwamuzi huyo ameeleza hayo wakati aki-chat Instagram na Semaji la Dunia Haji Sunday Manara.
Mwamuzi Beida Dahane ameweka wazi kuwa wakati wa faulo ya Lomalisa wanao-control VAR walishindwa kutoa maamuzi hivyo walihitaji msaada wake ndio maana alienda kuwasaidia lakini Kwenye Goli la Aziz Ki hakwenda kuthibitisha kwenye VAR kwa sababu haikuwa kazi ngumu kwa wanao-control VAR kutoa maamuzi, walimueleza mapema kuwa sio goli, hivyo kama kuna makosa yoyote walaumiwe wao.
Mwamuzi Beida Dahane amefunguka kuwa hawezi kuomba msamaha kwa Watanzania kwani hakuhusika katika maamuzi, kama kuna kosa lolote amefanya basi ataomba msamaha kwa Mungu.
Mwamuzi Beida Dahane amesisitiza kwamba yeye ndiyo anatakiwa kuombwa msamaha maana anashambuliwa sana kutokana na sakata hili, wakati wanaotakiwa kushambuliwa ni watu wa VAR.