MPANGO WA PARIS ST-GERMAIN KWA VICTOR OSIMHEN

0:00

MICHEZO

Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris St-Germain wamepaga kulipa Pauni 111.5 milioni kumnunua Mshambuliaji wa SSC Napoli, Victor Osimhen katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Staa huyo wa kimataifa wa Nigeria kwenye mkataba wake kuna kipengele ambacho kinamruhusu kuondoka ikiwa timu inayomtaka italipa kiasi hicho cha pesa.

PSG imekuwa ikimuwinda nyota huyo tangu dirisha lililopita la majira ya kiangazi, ili awe mbadala wa mshambuliaji Kylian Mbappe ambaye ataondoka mwisho wa msimu huu.

Osimhen alivivutia vigogo vingi barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu msimu uliopita ambapo alikuwa mfungaji bora wa Serie A akiwa na mabao 26.

Katika msimu huu licha ya SSC Napoli kutofanya vizuri, Osimhen ameendelea kufanya vizuri ambapo amefunga mabao 13 kwenye mechi 25 za michuano yote.

Chelsea na baadhi ya timu za Saudi Arabia pia zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili staa huyo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Euro 2024 was not just a historic...
Four stalwarts - Ilkay Gundogan, Thomas Muller, Manuel Neuer and...
Read more
President Bola Tinubu says his administration will...
The President stated this while receiving a presentation titled, ‘Harnessing...
Read more
BASHUNGWA AMPA MKANDARASI MIEZI MIWILI KUKAMILISHA UJENZI
HABARI KUU Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa miezi miwili...
Read more
WOMAN BERATES THOSE ADVISING CHIOMA TO LEAVE...
CELEBRITIES American woman chides those advising Chioma to leave Davido...
Read more
TAARIFA YA PACOME ZOUZOUA KWA SASA
MICHEZO Kiungo wa klabu ya Yanga, Pacome Zouzoua ambaye alipata...
Read more
See also  WACHEZAJI NYOTA WALIOWAHI KUKATAA KUSAJILIWA NA REAL MADRID

Leave a Reply