MWAMUZI BEIDA DAHANE APATA ULAJI FIFA

0:00

MICHEZO

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limemteua mwamuzi Beida Dahane aliyechezesha mchezo kati ya Young Africans Sc dhidi ya Mamelodi Sundowns kuchezesha michezo ya soka ya mashindano ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.

Dahane (32) ambaye alisimamia mchezo huo ulioishuhudia Yanga ikiondolewa kwenye hatua ya robo fainali kwa penalti 3-2 ni miongoni mwa waamuzi 12 kutoka Afrika ambao wamepata fursa hiyo huku kiujumla wakiteuliwa marefa 89 kutoka nchi tofauti duniani.

Katika mchezo huo uliopigwa Aprili 5, 2024, Dahane alizua gumzo baada ya kukataa bao la kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambalo kwa mujibu wa baadhi ya picha za video na za mnato, mpira ulivuka wote mstari wa goli ingawa kwa uamuzi wa refa, haukuvuka wote.

Waamuzi kutoka Afrika walioteuliwa kuchezesha michezo ya Olimpiki mwaka huu ni Karboubi Bouchraw wa Morocco, Mahmood lsmail (Sudan), Diana Chkotesha (Zambia), Fatiha Jermoumi (Morocco), Elvis Noupue (Cameroon), Stephen Yiembe (Kenya), Mahmoud Ashour (Misri), Lahlou Benbraham (Algeria), Ahmed Abdoulrazack (Djibouti), Emiliano Dos Santos (Angola) na Shamirah Nabadda Uganda).

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Men’s doubles pair Aaron Chia-Soh Wooi Yik...
World No. 5 Satwiksairaj-Chirag started aggressively but Aaron-Wooi Yik turned...
Read more
WIMBO MPYA WA ZUCHU "SIJI"
Read more
Wabunge Waonywa Kuwa Makini na Ma Gen...
NAIROBI, Kenya - Seneta wa Meru Kathuri Murungi amewashauri wabunge...
Read more
Stalemate at National Consultative Council Meeting in...
A stalemate has erupted at the National Consultative Council (NCC)...
Read more
MCTominay earns leaders Napoli win at Torino
A first-half goal by Scott McTominay earned leaders Napoli a...
Read more
See also  BORUSSIA DORTMUND YAICHAPA BAYERN MUNICH BAADA YA MIAKA 10

Leave a Reply