0:00
MAPENZI
- Kuna mwanamke ambaye akikasirika, huishia kulia tuu!
- Lakini mwingine akichukia, anaongea saanaa muda wote hadi ikukere!
- Mwanamke mwingine akikasirika, ananuna, haongei! Mtapishana tu kimya kimya. Mawasiliano kibubu-bubu. Shavu limejaa kama Kobra!
- Mwingine akishikwa na hasira, period ya ghafla ghafla inafuata!
- Wako wanawake ambao, ole achukie! Atakachokishika usipokimbia anakutandika nacho, majuto baadaye!
- Mwanamke mwingine akikasirika, hasira zake zinaishia kwenye kuvunja-vunja vyombo. Au saa nyingine kugombeza-gombeza wafanyakazi na watoto! Dizaini hii, huwa ni wale waliokosa kukidhiwa haja za kihisia na waume zao!
- Mwanamke mwingine ole akasirike. Mtajuana kitandani panapo majaaliwa! Nakwambia utaungama yote!
- Kuna ambao wakitibuliwa, hukimbilia kufunga mabegi na kuondoka!
- Wapo ambao wakikasirika, wanagoma kupika!
- Wengine wakichukia, wanaamua kwenda kulala kimyaaa!!
- Wanawake wengine wakikasirika, tumbo linakata na kichwa kuwauma
- Wako ambao wakishikwa na hasira, huingia maombi na kuugua kusikoweza kutamkwa. Uchungu ukiisha, wananawa uso wao
- Yuko ambaye akishikwa na hasira, hucheka saaanaaa…. Hutajua kama amekasirika! Dizaini hii ni hatari sana, maana anaweza kukudhuru kiurahisi.
- Wapo ambao hukimbilia kuwaambia ndugu zake yaani kueleza ili waseme kitu
Related Posts 📫
MICHEZO
Klabu ya Manchester United imewekeza nguvu kubwa zaidi kwenye...
MICHEZO
Arsenal imetikiswa baada ya beki wake mahiri kabisa, Gabriel...
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali iko mbioni...
On Sunday morning, a fire erupted at the Christ Embassy...
Director Pink, a renowned Nigerian music video director, has strongly...