FISTON MAYELE AFUNGUKA MAZITO BAADA YA KUONDOKA TANZANIA

0:00

NYOTA WETU

Mshambuliaji wa Pyramids FC ya Misri, Fiston Mayele akifanya mahojiano na kituo cha habari cha Azam, ameeleza kuwa kocha aliyemkuta ndani ya kikosi cha Pyramids wakati anatokea Yanga Sc alitaka kumtoa kwa mkopo Disemba 2023 lakini Rais wa Klabu hiyo alizuia jambo hilo na kumuondosha kocha huyo.

“Wakati nakuja Pyramids kocha niliyemkuta alikuwa na wachezaji wake, na mimi nikaingia kuna wakati alinichezesha nilikuwa natoa assist au nafunga najua mechi hii nimefanya vizuri hivyo mechi ijayo nitaanza, mechi inakuja ananiweka tena nje.

“Ulifika wakati nikaenda kuongea na viongozi wa timu nikawaambia sikuja Pyramids kukaa nje kama mnaona mnaniweka nje Disemba (Disemba 2023) naondoka, niliwaambia hapa nimekuja kucheza.

“Disemba tulienda kucheza Kombe la Uarabuni na tukafungwa, baada ya ile mechi yule kocha akaandika list ya wachezaji wakutolewa kwa Mkopo jina langu lilikuwa la kwanza kwenye list, Rais wa timu akamwambia sawa tutakujibu.

“Mimi nikiwa AFCON yule Rais akanipigia akaniambia jina lako limetolewa huku utolewe kwa mkopo lakini siwezi kukubali kwasababu naamini utaisaidia timu yangu akaniambia mimi nitamuondoa yeye (Kocha), Rais akamuondoa yule kocha,” Mayele.



Fiston Mayele amesema pia baada ya Pyramids kumtambulisha kama mchezaji wao mpya kesho yake aliamka na kukuta mguu wake umevimba hivyo alifunga safari kurejea Tanzania hadi kwa Nabii, Boniface Mwamposa kufanyiwa maombi.

“Baada ya ile mechi ya dodoma nililia sana niliumia mguu ulivimba hata kutembea sikuweza, hospitali walisema nimevunjika lakini hawawezi kuniweka hogo maana mguu umevimba utaoza alafu watanikata hivyo natakiwa nikae tuu hadi mguu upungue, nikaanza kuwaza vitu vingi nikasafiri kwenda Congo.

“Nilivyoenda Congo Mungu akasaidia nikawa sawa nikaenda Pyramids kusaini walivyonitambulisha kesho yake nikaamka mguu umevimba tena nikasema hapana, nikarudi tena Congo Kisha Tanzania nikaenda kwa Mwamposa akanisaidia mguu ukarudi kidogo.

“Mpaka Leo mguu wangu mmoja umevimba haujarudi kama zamani, hakuna maumivu Lakini mguu mmoja ni mkubwa kuliko mwingine,” Mayele.

See also  WATOTO WA MR IBU WAIBA PESA ZA MICHANGO YA MATIBABU

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Russia's Valieva plans to resume career after...
Russian figure skater Kamila Valieva plans to resume her competitive...
Read more
YANGA KUFUATA STRAIKA ULAYA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
WHO IS THOMAS FULLER "Negro Tom" and...
Thomas Fuller, also known as "Negro Tom" and the "Virginia...
Read more
5 HARDEST PART OF MARRIAGE YOU WON'T...
LOVE TIPS ❤ Marriage is sweet when you examine it...
Read more
Bournemouth have agreed a club record £40.2m...
They will pay £31.7m with the potential for another £8.5m...
Read more

Leave a Reply