UJUMBE WA MSEMAJI WA SIMBA AHMED ALLY HUU HAPA

0:00

NYOTA WETU

… 🧠 𝗔𝗨 𝗠𝗜𝗠𝗜 𝗡𝗗𝗜𝗢 𝗦𝗜𝗘𝗟𝗘𝗪𝗜 ?

Nimewasikia wachambuzi kadhaa wakisema Simba SC imebakiza points (4) imfikie kinara wa ligi Yanga SC.. Nilidhani labda ni kupitiwa.

Baada ya kauli ya Ahmed Ally ndipo nikagundua sio kupitiwa, labda mimi pekee ndio nina msimamo tofauti wa ligi.

1. 👕 20 ⚽ +38 🅿️ 52 — Yanga
2. 👕 21 ⚽ +31 🅿️ 47 — Azam FC
3. 👕 19 ⚽ +21 🅿️ 45 — Simba

52 – 45 = 7 Kwa nini ni (4) ?!

Au tunahesabu points za mechi ya Ihefu ambayo haijachezwa ?!



“Timu yetu inapitia kipindi kigumu Lakini ni tofauti na inavyozungumzwa yaani ugumu unaoelezwa ni tofauti na uhalisi yaani wanaongeza chumvi”

Huu ni mpango wa makusudi unaoratibiwa na wasiotutakia mema, Bahati mbaya ni kwamba Wana Simba tumeingia kwenye mtego wa kujidharau na kujitukana

Tukiwa na Simba Bora sana tuliwahi kutolewa hatua ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika na UD Songo, Tukiwa na Simba Bora tuliwahi kutolewa na Green Warrios kwenye Kombe la Shirikisho

Haya mi Maisha ya kawaida kwenye mpira wa miguu

Kila timu ya mpira hupitia nyakati kama hizi, Ila tukipitia Simba basi huonekana ni kitu cha ajabu inawezekana tunahukumiwa na ukubwa wetu

Wana Simba tunakubali kucheza ngoma ya wabaya wetu, Leo watakuambia wachezaji wabovu, kesho Muwekezaji tatizo, kesho kutwa Viongozi hawafai

Hivi tungekua na matatizo yote hayo si tungekua tumeshuka daraja?

Wengine wanaibuka kukashifu viongozi na kudhihaki wachezaji wakiamini huko ndio kuipenda Simba au wao ndio wenye uchungu sana na Simba

Acha niwakumbushe wakati Nyuma Mwiko wako dhofli hali waliibuka na kauli ya kusema tumeipenda wenyewe acha ituue, Hii ilikua kauli ya kishujaa sana na waliamua kufa na timu yao

Kwa sasa hatuna budi kusimama na timu yetu ili mambo yasiharibike zaidi, hatuwezi kubadili yaliyopita ila tunaweza kutengeneza yajayo

“Tulichobakiwa nacho ni Ligi Kuu ya NBC, Kwa pamoja tuwekeze nguvu kwenye kombe hili”

“Tuache kulaumiana, tuhamishie machungu yetu na tuelekeze hasira zetu kwenye ligi”

“Pengo ni alama 4 tukisimama sawa sawa kwa umoja wetu tunaliondoa”

“Hii inaanza na mechi ya Tarehe 13 dhidi ya Ihefu, na baada ya hapo mechi ya tarehe 20, tukichukua alama 6 kwenye mechi hizi tutakua pazuri sana Kuelekea Ubingwa”

“FID Q alisema nipeni heshima yangu au niichukue kwa nguvu, Twendeni tukaichukue heshima yetu kwa nguvu…”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  MCHEKESHAJI WA NIGERIA "MR IBU" APATWA NA MKASA MZITO

Related Posts 📫

MANCHESTER CITY NA ARSENAL HAKUNA MBABE
MICHEZO Mbio za kuwania taji la EPL zimezidi kupamba moto...
Read more
Fanya Mambo Haya Kwa Wale Wanawake Ambao...
Kwanza kutongoza kunaweza kua kwa aina nyingi hivyo nianze kwa...
Read more
MBUNGE AIBUA MAZITO KINACHOENDELEA NGORONGORO ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Fenerbahce's Mourinho suspended and fined for comments...
Fenerbahce coach Jose Mourinho has been suspended for one match...
Read more
ROBERTINHO KWANINI AFUKUZWE? ...
Michezo Tangu jana nimekuwa nikifatilia mijadala sana inayojiri kwenye mitandao...
Read more

Leave a Reply