UJUMBE WA MSEMAJI WA SIMBA AHMED ALLY HUU HAPA

0

0:00

NYOTA WETU

… ๐Ÿง  ๐—”๐—จ ๐— ๐—œ๐— ๐—œ ๐—ก๐——๐—œ๐—ข ๐—ฆ๐—œ๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐—ช๐—œ ?

Nimewasikia wachambuzi kadhaa wakisema Simba SC imebakiza points (4) imfikie kinara wa ligi Yanga SC.. Nilidhani labda ni kupitiwa.

Baada ya kauli ya Ahmed Ally ndipo nikagundua sio kupitiwa, labda mimi pekee ndio nina msimamo tofauti wa ligi.

1. ๐Ÿ‘• 20 โšฝ +38 ๐Ÿ…ฟ๏ธ 52 โ€” Yanga
2. ๐Ÿ‘• 21 โšฝ +31 ๐Ÿ…ฟ๏ธ 47 โ€” Azam FC
3. ๐Ÿ‘• 19 โšฝ +21 ๐Ÿ…ฟ๏ธ 45 โ€” Simba

52 – 45 = 7 Kwa nini ni (4) ?!

Au tunahesabu points za mechi ya Ihefu ambayo haijachezwa ?!



“Timu yetu inapitia kipindi kigumu Lakini ni tofauti na inavyozungumzwa yaani ugumu unaoelezwa ni tofauti na uhalisi yaani wanaongeza chumvi”

Huu ni mpango wa makusudi unaoratibiwa na wasiotutakia mema, Bahati mbaya ni kwamba Wana Simba tumeingia kwenye mtego wa kujidharau na kujitukana

Tukiwa na Simba Bora sana tuliwahi kutolewa hatua ya awali ya ligi ya Mabingwa Afrika na UD Songo, Tukiwa na Simba Bora tuliwahi kutolewa na Green Warrios kwenye Kombe la Shirikisho

Haya mi Maisha ya kawaida kwenye mpira wa miguu

Kila timu ya mpira hupitia nyakati kama hizi, Ila tukipitia Simba basi huonekana ni kitu cha ajabu inawezekana tunahukumiwa na ukubwa wetu

Wana Simba tunakubali kucheza ngoma ya wabaya wetu, Leo watakuambia wachezaji wabovu, kesho Muwekezaji tatizo, kesho kutwa Viongozi hawafai

Hivi tungekua na matatizo yote hayo si tungekua tumeshuka daraja?

Wengine wanaibuka kukashifu viongozi na kudhihaki wachezaji wakiamini huko ndio kuipenda Simba au wao ndio wenye uchungu sana na Simba

Acha niwakumbushe wakati Nyuma Mwiko wako dhofli hali waliibuka na kauli ya kusema tumeipenda wenyewe acha ituue, Hii ilikua kauli ya kishujaa sana na waliamua kufa na timu yao

Kwa sasa hatuna budi kusimama na timu yetu ili mambo yasiharibike zaidi, hatuwezi kubadili yaliyopita ila tunaweza kutengeneza yajayo

“Tulichobakiwa nacho ni Ligi Kuu ya NBC, Kwa pamoja tuwekeze nguvu kwenye kombe hili”

“Tuache kulaumiana, tuhamishie machungu yetu na tuelekeze hasira zetu kwenye ligi”

“Pengo ni alama 4 tukisimama sawa sawa kwa umoja wetu tunaliondoa”

“Hii inaanza na mechi ya Tarehe 13 dhidi ya Ihefu, na baada ya hapo mechi ya tarehe 20, tukichukua alama 6 kwenye mechi hizi tutakua pazuri sana Kuelekea Ubingwa”

“FID Q alisema nipeni heshima yangu au niichukue kwa nguvu, Twendeni tukaichukue heshima yetu kwa nguvu…”

Mujuni Henry
See also  6 COMMON MISTAKES MEN MAKE IN BED
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading