NYOTA WETU
Msanii Harmonize ameingia katika mzozo na waumini wa dini ya Kiislamu huku wakimtaka afute mara moja maneno yake alioandika akimfananisha Mwenyezi Mungu na Mwanamke.
Kwa mujibu wa kile alichoandika kupitia Insta Story yake leo, Msanii huyo anasema imemchukua miaka 30 kugundua ya kuwa pengine Mungu ni Mwanamke kwa asilimia Kubwa.
Mmoja ya waumini wa Dini ya Kiislamu Sheikh Masoud akizungumza amemtaka Harmonize kufuta haraka maandishi hayo akisema Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa imani ya dini ya Kiislamu ambayo Harmonize ni muumini wa dini hiyo, hafananishwi na chochote.
“Huu ni msiba mkubwa kwa kijana wetu Harmonize” Anasema Masoud kutoka Altamimy Travel tz moja ya Kampuni ambazo zimekuwa zikipeleka mahujaji Makka.
“Anapaswa afute haraka mno maneno haya” amesema Masoud✍️