HABARI KUU
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema atawataja kwa majina wote wanaohusika kuwalipa watu kwaajili ya kumtukana Rais kwenye mitandao ya kijamii.
“Nafahamu wenye maneno hawaishi kusema maneno, lengo lao ni kukatisha tamaa, tena wengine umetupa nafasi tumo ndani ya uongozi wako na nitumie fursa hii kuwaambia hasa kaka zangu mnaotuma watu na kulipa kuchokoza mama yangu, ninawajua na ninyi mnanijua narudia tena hasa kaka zangu mnaotuma watu na kulipa kuchokoza mama yangu Samia, Mheshimiwa Rais kwa majina yao nawajua na leo tarehe 12 nataka iwe mwisho kuwatuma watu wao wanaokutukana kwenye mitandao ya kijamii, Jumatatu ikiendelea Jumatatu ninakutajia majina, wengine ni Mawaziri na wengine wanapewa nguvu na watu tunaowaheshimu naomba iwe mwisho.”-
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameyasema hayo kwenye kumbukumbu ya miaka 40 ya hayati Moringe Sokoine.