NYOTA WETU
Diamond Platnumz amesema shoo za Nigeria anazikataa mara kibaio, kwa sababu wanajua ukubwa wake ila wanachukulia poa.
“Unajua mimi sijafanya shoo Nigeria muda mrefu kwa sababu wana tabia ya ‘ku-understimate’ ukubwa wako licha ya kujua nguvu yako. Shoo nyingi nimezikataa kwa sababu nataka kiasi hiki wao wanataka kipungue. Unataka nije kwenye shoo yako nichukulie ‘private jet’ nitakuja, hutaki pita hivi siji kwenye hiyo shoo kwanza siwezi kosa hela ya kula,” ndivyo alivyoanza kufunguka.
Mbali na hilo pia Diamond akaongelea uwepo wa ‘kolabo’ zake na wanamuziki wengi wa Kimarekani.
Akisema hivi:
“Unajua ‘kolabo’ za kimataifa hazitokagi tu hovyo, mimi nina nyimbo na watu wengi, na wasanii wa Marekani ninazo nyingi sana. Na sasa hivi ilivyo, Wamerakani wanapenda sana kufanya nyimbo na wasanii wa Afrika. Sisi Waafrika tumekuwa dili. Na page yangu ya Instagram sasa hivi nimeweka kimkakati sana yani ‘nikimdiem’ msanii wa Marekani ‘Hey it’s Diamond Platnumz’ hachomoi.”
Huyo ni Diamond mapema hii leo alipozungumza na wanahabari.