SABABU ZA KLABU YA YOUNG AFRICANS KUFUNGIWA KUSAJILI NA FIFA

0

0:00

MICHEZO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuwa Klabu ya Young Africans (Yanga) inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Taarifa imeeleza kuwa uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Aidha Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika (jina halijatajwa) katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Yanga imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya
Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  VICTOR OSIMHEN KUAMIA LIGI YA ENGLAND
Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading