HABARI KUU
Diwani wa Kata ya Sinoni, Michael Kivuyo amesema Wananchi wakishirikiana na Kikosi cha Uokozi wanashiriki zoezi la kutafuta Wanafunzi 7 ambao hawajulikani walipo baada ya Gari la Shule ya Ghati Memorial kuanguka kwenye korongo, Asubuhi ya leo Aprili 12, 2024
Amesema
“Waliokuwa kwenye gari ni Wanafunzi 11, Dereva na Matroni. Wanafunzi Watatu, Dereva na Matroni wameokolewa, mwili mmoja umepatikana, Wananchi wameingia mtoni, wengine wamepewa usafiri kufuata uelekeo wa mto ili kuwatafuta ambao hawajapatikana.”
Inadaiwa Dereva wa gari la shule alipofika eneo la tukio alionywa na Bodaboda kutopita wakimsisitiza kuwa kasi ya maji ni kubwa, akalazimisha kupita akiwaambia alipita hapo awali kabla ya kuwabeba Wanafunzi. Baada ya ajali na dereva kuokolewa, Bodaboda hao wakaanza kumshambulia kwa kumpiga, akaokolewa na Wasamaria wema