HABARI KUU
Iran imefanya shambulizi kubwa dhidi ya Israel usiku wa kuamkia hii leo Aprili 14, 2024 kwa mamia ya ndege zisizo na rubani zinazodaiwa kufikia 300 na makombora ya balestiki katika mzozo wao wa kikanda.
Ushahidi wa Video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha makombora ya Iran juu ya msikiti wa Al-Aqsa jijini Jerusalem au juu ya Bunge la Israel .
Shambulio hilo, linadaiwa kujumuisha makombora 110 ya balestiki, makombora 36 ya cruise na ndege zisizo na rubani 185 ambapo Israeli inasema asilimia 99 ya vifaa ambavyo vilikuwa hatari vimeshaangamizwa.
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema wanajipanga kujibu mashambulizi ya tukio hilo la mara ya kwanza tangu vita vya kwanza vya Ghuba kwa Israel kushambuliwa na taifa huru kwa wakati huo, mwaka wa 1991.