MICHEZO
Ikicheza mchezo wake wa 21, Yanga imepata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza
Magoli yamefungwa na Joseph Guede mawili na Stephene Aziz Ki, hivyo Yanga imefikisha pointi 55, ikiongoza kwa tofauti ya pointi 8 dhidi ya Azam FC inayofuatia ikiwa na pointi 47 kisha Simba alama 46
Ushindi huo unaiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, mchezo ujao ikitarajiwa kukipiga dhidi ya Simba kwenye Kariakoo Derby.