KOCHA MIGUEL GAMONDI ATAJA ORODHA YA WACHEZAJI WATAKAOACHWA YOUNG AFRICANS

0:00

MICHEZO

Taarifa kutoka ndani Young Africans ni kwamba kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi kawasilisha mapema ripoti kwa mabosi wa klabu hiyo ikiwa ni mikakati ya kuanza kukisuka upya kikosi cha msimu ujao.

Hesabu za Gamondi zimeonyesha kuhitaji kuongeza kipa mmoja atakayechukua moja ya nafasi ya makipa watatu waliopo sasa akiwamo Djigui Diarra, Metacha Mnata na Aboutwalib Mshery. Mmoja kati ya hawa atapewa mkono wa kwaheri.

Kwenye ukuta hasa eneo la mabeki ripoti hiyo imeonyesha kuhitaji beki mmoja wa kushoto ambapo hapa kuna uwezekano mkubwa kwa mkongwe Joyce Lomalisa akapewa mkono wa kwaheri kwani mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu.

Ripoti hiyo, inaelezwa pia inahitaji kiungo mkabaji mwenye ubora zaidi au sawa na Khalid Aucho atakayejiunga kikosini kusaidiana na Mganda huyo pamoja na Jonas Mkude aliyepindua meza kibabe kwa kubakishwa baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi mbili dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Gamondi pia inaelezwa anahitaji winga mmoja na mshambuliaji wa maana watakaokuja kuongeza nguvu kwenye eneo la mwisho ambalo bado mshambuliaji Joseph Guede ameanza cheche akifunga dhidi ya Singida Fountain Gate.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Rais Samia atoa ujumbe mzito kwa viongozi...
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo kwenye...
Read more
PUSSY LOCKING: How to lock your pussy...
What is pussy locking? Don't think pussy locking is when you...
Read more
Nape Nnauye Ameponzwa na Mdomo au Utendaji...
MAKALA Usiku wa kuamkia leo Jumatatu tumefikiwa na taarifa za kutoka...
Read more
"WHY ARE MEN JUMPING ON THE 'ESTHER...
OUR STAR 🌟
See also  Why Rabbits are the best livestock to Farm.
"Why are men jumping on the 'Esther'...
Read more
Ni mazingira yapi Rais wa Tanzania anaweza...
Kwa mujibu wa Ibara ya 90(2) ya Katiba ya Jamhuri...
Read more

Leave a Reply