HABARI KUU
Mahakama kuu kanda ya Manyara imefutilia mbali rufaa ya Hashimu Ally dhidi ya Mbunge wa jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul kwa sababu Rufaa hiyo haikuwa na mashiko mbele ya mahakama hiyo
Maamuzi hayo yametolewa na Jaji wa mahakama kuu kanda ya Manyara Devotha Kamzola huku akiwataka warufani kukata rufaa kama hawajaridhika na maamuzi hayo
Kwa Upande wake wakili wa Hashimu Ally, Peter Madeleka amesema kuwa hajaridhishwa na maamuzi hayo kwani kuna madudu yanaendelea kwenye kesi hiyo hivyo ndani ya siku mbili watahakikisha wanakata rufaa kwenda mahakama ya Rufaa ili haki dhidi ya mteja wake itendeke
Naye wakili wa Pauline Gekul , Efrem Kisanga amesema kuwa maamuzi yaliyotolewa na Jaji Devotha mbele ya mahakama kuu kanda ya Manyara ni maamuzi sahihi hivyo muda wowote kuanzia sasa mteja wake atafungua kesi ya maadai kwa wale wote waliomchafúa kupitia Kashfa hiyo na ukweli wote utajulikana ndani ya musa mfupi
Ikumbukwe Kuwa Pauline Gekul àlifikishwa mahakama ya wilaya ya Babati kwa Kesi ya kumuingizia chupa ñyuma ya maumbile aliyekua mfanyakazi wake Hashimu Ally na kesi hiyo kutupitiliwa mbali na Mkurugenzi wa Mashtaka kutokana na mamlaka aliyopewa
Hii ni Mara ya Pili Pauline Gekul kushinda kesi hiyi licha ya mrufani wake kutaka kukata rufaa kwenye mahakama ya rufaa
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.