ALEJANDRO GARNACHO NA TEN HAG WAINGIA KWENYE MGOGORO

0:00

MICHEZO

Manchester United wanaamini mshambuliaji kinda wa timu hiyo, Alejandro Garnacho amejiweka mbali na ugomvi ambao ungetokea kati yake na kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag baada ya nyota huyo kuunga mkono habari kwenye mtandao wa kijamii inayomkosoa kocha huyo.

Ingawa kwa mujibu wa chanzo kimoja kutoka ndani ya klabu hiyo bado mshambuliaji huyo anaweza kushughulikiwa na kocha huyo kutoka Uholanzi.

Mtandao wa kijamii ulimkosoa Ten Hag namna alivyokitathmini kiwango cha Garnacho kwenye sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bournemnouth Jumamosi (Aprili 13) na mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina kuunga mkono habari hiyo.

Kwa mujibu wa ESPN, Garnacho haraka aliondoa alama hiyo ya kuonesha kuunga mkono kukosolewa kocha huyo, huku chanzo hicho kikisema hatua yoyote anayoweza kuchukuliwa chipukizi huyo inachukuliwa kuwa mambo ya ndani kwenye klabu hiyo.

Kwenye mchezo huo, Garnacho alifanyiwa mabadiliko wakati wa mapumziko baada ya kupokonywa mpira uliozaa bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji wa Bournemouth, Dominik Solanke. Bao la pili la Bournemouth lililofungwa na Justin Kluivert pia lilitokea upande wa kulia ambao alicheza Garnacho.

Alipoulizwa baada ya mechi hiyo kwanini alimfanyia mabadiliko Garnacho wakati wa mapumziko, Ten Hag alijibu: “Nafikiri tulikuwa kurekebisha upande wa kulia. Na tukucheza vizuri, tuliacha nafasi tukiwa kwenye umiliki wa mpira, tulikuwa kufanya mabadiliko kule,”

Ten Hag pia alisema Garnacho hakuwa sawasawa kabla ya kuchaguliwa kuanza mchezo huo.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Devoted Arsenal supporter ended his life after...
SPORTS Devoted Arsenal supporter ended his life after the team’s...
Read more
MAMBO MAKUU 4 YA KUZINGATIA KABLA YA...
MAPENZI
See also  Roberto De Zebri kwenye rada za Bayern Munich
Fahamu mambo 4 muhimu unayopaswa kuyazingatia uwapo chumbani na...
Read more
Things that ruins sex for a lady
LOVE TIPS ❤ THINGS THAT RUINS S3X FOR A LADY;...
Read more
Adam Peaty has tested positive for Covid-19...
Peaty missed out on a third consecutive gold medal by...
Read more
Nchini Korea Kaskazini kama "Birthday" yako ni...
Sababu kubwa ni kwamba tarehe hizo Baba wa Taifa hilo...
Read more

Leave a Reply