HABARI KUU
Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya Hajirat Shabani (22) mwanafunzi wa chuo cha St. Joseph kilichopo mkoani Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro SCAP. ALex Mkama amesema tukio limetokea tarehe 16 aprili mwaka huu nje ya hosteli za chuo hicho alipokuwa akiishi Hajirat ambapo watuhumiwa hao walimvamia marehemu kwa lengo la kumpora simu wakati marehemu akimzuia kuporwa simu yake ndipo mtuhumuwa mmoja alichomoa kisu na kumchoma sehemu mbalimbali za mwili wake na jambo lililopelekea kupoteza maisha.
RPC Mkama amewataja watuhumiwa hao waliokamwata ni Tyson Eliakim (20) ndiye alimchoma kisu marehemu , mwingine ni Elias Lenjemet (29) alikuwa bodaboda siku ya tukio pamoja Fedrick Nongwa (21) mmiliki wa pikipiki namba MC 285 EDX ambayo ilitumika siku ya tukio.
Kamanda mkama amesema kuwa Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.