AFYA

MADHARA YA FANGASI UKENI👇

Madhara yafuatayo yanaweza kutokea ikiwa mgonjwa mwenye fangasi ukeni atashindwa kupata tiba mapema;

⏩ Mimba Kuharibika.

Hii hutokea kwa mama mjamzito ambaye hakupata tiba ya maambukizi ya fangasi ukeni mapema ambapo maambukizi hayo huenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kuharibu mji wa mimba (uterus),

sehemu ambapo mimba hujishikiza (fetal implantation) na kupelekea mimba kuharibika kabla ya wakati wake.

⏩Kupata Homa Na Kizunguzungu.

Hali hii hutokea kwa sababu ya kubadilika kwa hali ya kawaida ya mwili

na kuharibika kwa sehemu mbalimbali za mwili kutokana na maambukizi ya fangasi hali ambayo husababisha kubadilika kwa joto la mwili pia.

⏩ Kuongezeka Kwa Miwasho Sehemu Za Siri.

Madhara ya fangasi ukeni husababisha kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu za siri ambapo mwathirika hujikuna kila wakati,

hali hii huongeza uwezekano mkubwa wa kuenea kwa ugonjwa wa fangasi ukeni

kwa sababu mwenye maambukizi kama anajikuna na anawagusa wengine wanaomzunguka basi anaweza kusambaza maambukizi hayo kwa wanaomzunguka kwa urahisi.

⏩Maumivu Makali Wakati Wa Kukojoa.

Hali hii hutokea kwa mgonjwa Mwenye tatizo la fangasi ukeni,

pale ambapo maambukizi yameenea sehemu mbalimbali za via vya uzazi na kusababisha michubuko.

Hivyo wakati wa haja ndogo, mgonjwa akikojoa na mkojo ukagusa sehemu ya michubuko maumivu makali hutokea na kusababisha kukosa raha.

JINSI YA KUJIKINGA NA FANGASI UKENI👇

Yafuatayo ni mambo ya muhimu ambayo mwanamke anapaswa kuzingatia ili kujikinga na fangasi ukeni;

✅Vaa nguo za ndani ambazo hazibani na zilizotengenezwa kwa pamba au hariri.

✅Epuka kufanya mapenzi na mpenzi wako mwenye maambukizi haya mpaka pale atakapotibiwa na kupona kabisa.

✅Osha sehemu zako za siri kwa kutumia maji safi na jikaushe kwa kutumia taulo au kitambaa safi.

✅Epuka kuoga maji ya moto sana (hot baths), tumia maji ya vuguvugu.

✅Kula mlo wenye virutubisho kama vile mboga za majani, matunda.

✅Kunywa maziwa aina ya
yenye live culture mara kwa mara yatakusaidia.

✅Epuka matumizi ya vifaa vya kupanga uzazi na vifaa vya kufanyia mapenzi (sex toys, diaphragm, cervical caps) husababisha maambukizi ya fangasi ukeni.

✅Epuka kutumia sabuni za kemikali au dawa kuoshea uke.

✅ Usivae nguo zenye unyevunyevu, hakikisha unavaa nguo zilizokauka vizuri.

✅ Epuka kutumia kiholela dawa za Antibiotics, kama huna ulazima wa kutumia antibiotics, acha kutumia.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.