AFYA
Kuwashwa sehemu za siri kwa wanawake ni miongoni mwa changamoto za kiafya zinazowasumbua wanawake wengi bila kujali rika lao.
Tatizo la kuwashwa sehemu za siri kwa wanawake ni kubwa na hupelekea mwanamke kupata matatizo ya kisaikolojia kwa kuwa mara nyingi inakuwa vigumu wakati mwingine kusema kwa daktari kwamba nina tatizo sehemu zangu za siri.
Kuwashwa Sehemu Za Siri
Leo katika makala yetu tutazungumzia sababu zinazopelekea mwanamke kuwashwa sehemu za siri.
Sababu Zinazopelekea Mwanamke Kuwashwa Sehemu Za Siri:
Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazopelekea mwanamke kuwashwa sehemu za siri ambazo ni pamoja na;
1) Maambukizi Ya Fangasi Ukeni.
Maambukizi ya fangasi ukeni hujulikana kwa kitaalamu kama yeast infection. Maambukizi haya ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao candida albicans.
Dalili kuu za maambukizi haya ni pamoja na kuwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.
2) Ugonjwa Wa Kuvimba Uke.
Ugonjwa wa kuvimba uke hujulikana kwa kitaalamu kama vulvovaginitis.
Huu ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe.
Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.
3) Kuvimba Uke Baada Ya Hedhi Kukoma.
Kuvimba uke baada ya hedhi kukoma hujulikana kwa kitaalamu kama Postmenopausal Atrophic Vaginitis.
Huu ni ugonjwa wa kuvimba uke baada ya hedhi kukoma, hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha muwasho ukeni na maumivu wakati wa tendo la ndoa.
4) Maambukizi Ya Trikomonasi (Trichomoniasis).
Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomoniasis) ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu za ugonjwa huu ni pamoja na muwasho ukeni na kutokwa na uchafu ukeni.
5) Ugonjwa Wa Minyoo (Trichomonas Vaginalis)
Ugonjwa wa minyoo hujulikanao kwa kitaalamu kama pinworm infection ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa