YUSUPH MANJI AIBUKA AMTAJA KIGOGO ANAYEFANYA SIMBA KUTOKUFANYA VIZURI

0:00

MICHEZO

“Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati mgumu ni Hans Poppe. Huyu jamaa alikuwa anafanya kazi yake kuonesha kabisa kuwa Dabi inatakiwa kuwa na mvuto, alikuwa akizungumza na watu wanamuelewa, alinipa wakati mgumu sana.

“Hata niliposikia amefariki, ukweli kibinadamu nilisikitika sana kwa kuwa alikuwa ni mtu muhimu kwenye soka, lakini nilijua kabisa kuwa Simba inakwenda kupata wakati mgumu na hiki ndiyo kinatokea leo, nafikiri mechi umeiona na msimamo unaonesha hali halisi ilipo Yanga na Simba kwa sasa,” alisema Manji ambaye alidumu kwenye timu ya Yanga kwa miaka 13 kama mfadhili na Mwenyekiti.

“Tulikuwa tunapambana sana uwanjani, lakini tulikuwa marafiki, alikuwa akizungumza lazima nijue amesema nini, huyu alikuwa ana nguvu kubwa sana kwenye soka la Tanzania na alikuwa anaweza kufanya jambo lolote na watu wakamuelewa.”

“Nafikiri unakumbuka wakati tulipoichapa Simba mabao matatu hadi mapumziko, baadaye wakaja kurudisha yote. Hapa Hans Poppe alihusika, siwezi kukuambia alifanyaje, lakini nguvu yake ilisababisha Simba wakapata sare kwenye huo mchezo, alikuwa na ushawishi wa hali ya juu sana kwa wachezaji.”

Yusuph Manji – Mfadhili na Mwenyekiti wa zamani Young Africans

.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WHY ETHIOPIA IS SET TO JOIN EAST...
BREAKING NEWS Ethiopia is set to become the 9th...
Read more
SOME OF THE DARKEST SIDES OF WOMEN...
A woman can never love two men at the same...
Read more
Mwijaku atakiwa kulipa shilingi bilioni 5 kwa...
Wakili wa Masoud Kipanya mtangazaji maarufu ambaye pia ni mchambuzi...
Read more
Man handed a nearly 12-year prison sentence...
In a significant legal development, a Nigerian national has been...
Read more
KISA MRADI WA MAJI DKT MPANGO ATOA...
MAGAZETI
See also  MANCHESTER UNITED YAWEKA WACHEZAJI WAKE SOKONI
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more

Leave a Reply